Mbelewele : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 4:
'''Mbelewele''' ni punje zenye seli za kuzaa za kiume ndani ya [[maua]]. Zinapatikana kwenye chavulio juu ya stameni ya ua. Mbelewele ni lazima kwa mbegu wa mmea kujitokeza.
 
Mimea mingine huwa na mbelewele nyepesi inayosambazwa na upepo na kufikia kwenye kapeli ya ua.

Kuna aina nyingine yenye mbelewele nzitonzito inayonata ikiguswa. Aina hizi zina proteini na sukari hivyo zinapendwa kama chakula cha wadudu.

Kama [[mdudu]] kwa mfano [[nyuki]] au inzi anafikia ua anaanza kula au kukusanya mbelewele. Wakati wa kazi hii punje nyingi zinanata mwilini na mguuni wa mdudu anayezipeleka kwa maua mengine na kuzitungisha kwa njia hii.
 
Nyuki hukusanya mbelewele na kuipeleka kwenye [[mzinga wa nyuki]] inapotunza katika vyumba vya [[sega]]. Hapa inageukia kuwa [[asali]].