Daraja takatifu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: thumb|250px|Askofu akitoa upadrisho Katika Ukristo zinaitwa '''daraja takatifu''' vyeo vya askofu, kasisi na shemasi. Katika [[K...
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:Priestly ordination.jpg|thumb|250px|Askofu akitoaanatoa upadrishodaraja ya [[upadri]] akizungukwa na mashemasi]]
 
Katika [[Ukristo]] zinaitwa '''daraja takatifu''' vyeo vya [[askofu]], [[upadri|kasisi]] na [[shemasi]].
 
Katika [[Kanisa Katoliki]] na ya [[Waorthodoksi]] ngazi hizo tatu zinaunda kwa pamoja mojawapo ya [[sakramenti]] mojawaposaba ambazo [[Yesu Kristo]]alizianzishwa na kulikabidhi [[Kanisa]] lake.
 
Baadhi ya [[Waprotestanti]] wana huduma hizo lakini kwao si sakramenti.
 
==Jina==
 
Katika [[Kigiriki]] daraja zinaitwa ''taxeis'', na katika [[Kilatini]] ''ordines'', kwa sababu waliopewa wanaunda ''kundi'' moja.
 
==Ibada ilivyo==
 
Tangu zamani za [[Mitume]] mamlaka inashirikishwa kwa tendo la kumwekea mtu mikono kichwani, kufuatana na mfano wa [[Musa]] kwa [[Yoshua]] katika [[Agano la Kale]].
 
Tendo hilo linafuatana na sala maalumu ambayo, katika kumuomba [[Roho Mtakatifu]] amshukie mhusika, inaweka wazi daraja gani inatolewa.
 
==Anayetoa daraja==
 
Kwa kawaida mwenye jukumu la kutoa daraja takatifu ni askofu wa [[jimbo]] ([[dayosisi]]), ingawa [[historia ya Kanisa]] inasababisha maswali kadhaa juu ya jambo hilo hasa upande wa daraja za chini.
 
==Anayeweza kupewa==
 
Ni imani ya [[Kanisa Katoliki]], ya makanisa ya [[Waorthodoksi]] na ya madhehebu mengine kadhaa kwamba daraja zinaweza kutolewa kwa wanaume tu, kwa sababu [[Yesu]] aliteua watu wa jinsia hiyo tu awape mamlaka yake ambayo inashirikishwa kwa daraja hizo, na kwa sababu ndiyo [[mapokeo]] ya Kanisa tangu mwanzo.
 
Waprotestanti wanazidi kukubali wanawake katika nafasi zote za uongozi, wakisisitiza usawa wa wafuasi wa Yesu.
 
Katika Kanisa Katoliki na makanisa ya Waorthodoksi wanaopewa daraja wanaweza wakadaiwa pia hali na ahadi ya [[useja mtakatifu]]. Ni hivyo walau kuhusu uaskofu, lakini pengine hata kuhusu [[upadri]].
 
==Hali ya kudumu==
 
Sawa wa sakramenti za [[Ubatizo]] na [[Kipaimara]], katika [[imani]] ya Wakatoliki daraja takatifu zinamtia mwamini ''[[alama isiyofutika]]'' ya ki[[kuhani]] aweze kumtolea [[Mungu]] ibada katika liturujia na katika maisha yake yote.
 
Kwa maana hiyo daraja inadumu ndani ya mtu hata akiacha kutoa huduma au kuasi kabisa.
 
==Vyeo vingine visivyo sakramenti==
 
Katika madhehebu mbalimbali kuna vyeo tofauti na daraja takatifu, ambavyo vilianzishwa na Kanisa kulingana na mahitaji ya mahali na nyakati, kama vile vya [[Patriarki]], [[Kardinali]], [[Askofu mkuu]], [[Korepiskopo]], [[Paroko]], [[Vartan]], [[Mwenyekiti]] n.k.
 
Katika Kanisa Katoliki cheo cha kwanza ni kile cha [[Papa]] , ambacho kinategemea na kudai sakramenti ya daraja katika ngazi ya uaskofu kwa sababu ni kukabidhiwa jimbo la [[Roma]] kama mwandamizi wa [[Mtume Petro]] aliyefia huko.
 
Imani ya Kanisa hilo ni kwamba cheo hicho, ingawa si sakramenti, ni mpango wa Yesu aliyetaka mitume wake wawe kundi moja chini ya Petro, hivyo waandamizi wao wawe kundi moja chini ya mwandamizi wa Petro, yaani maaskofu wote duniani wawe kundi moja chini ya mkuu wao, askofu wa Roma.
 
[[Category:Ukristo]]