Isa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
(Hakuna tofauti)

Pitio la 17:59, 26 Machi 2005

Nabii Isa (AS)

Nabii Isa (AS) ni Mtume anayeaminiwa na Waislamu kama mmojawapo wa Mitume mitukufu wa Mwenyezi Mungu walioletwa kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu duniani, naye ni miongoni mwa Mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahmilivu wao mkubwa. Nao ni Manabii Nuhu na Ibrahim na Musa na Isa na Muhammad (amani na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao).

Nabii Isa (AS) ni mmojawapo wa 124,000 wa mfululizo wa Mitume na Manabii wa Mwenyezi walioletwa ulimwenguni kuwaletea ujumbe wanadamu wa Mwenyezi Mungu kuhusu upweke na umoja wake, na kumuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani. Watume na Manabii hawa wameletwa katika zama mbali mbali na kwa watu, kaumu na umma mbali mbali, na mfululizo huu ulianza na Adam (AS) baba wa wanadamu wote hadi Mtume Muhammad (SAW) akiwa ndiye wa mwisho katika Manabii na Mitume.

Kuzaliwa kwake

Nabii Isa (AS) alizaliwa na bibi Maryam kimiujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimletea Jibrili (AS) kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa (AS), alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwengine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mamake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba.

Ujumbe wake

Nabii Isa (AS) aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki, na ujumbe huu ndio ujumbe uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kupa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) ambao ndio ulikuwa wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote.

Salim Elhaj