Tofauti kati ya marekesbisho "Isa"

1,274 bytes added ,  miaka 16 iliyopita
no edit summary
 
'''Ujumbe wake'''
 
Nabii Isa (AS) aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki, na ujumbe huu ndio ujumbe uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kupa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) ambao ndio ulikuwa wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote.
 
'''Itikadi ya Kikristo kuhusu Isa (AS)'''
 
Wakristo au Manasara wanahitalifiana katika itikadi yao kuhusu Nabii Isa (AS), kwani kuna wanaomchukulia kuwa ni mtoto wa Mungu, na wengine wanaomuitakidi kuwa ni Mungu, na kuna kundi linalomchukulia kuwa ni Mtume au Nabii. Makundi haya yalitafautiana baada ya kuondoka Nabii Isa (AS) ulimwenguni na kuwawacha wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada yake, mbali na wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walikuja na fikra na mawazo mengine kuhusu Isa au Yesu kama anavyojulikana na Wakristo, na baada ya muda waligawanyika makundi mbali mbali, wakiwa wengine wanamuamini kuwa ni Mtume na Nabii kama alivyowafundisha na wengine wakawa wanamuamini kama ni mtoto wa Mungu au Mungu kwa sababu ya miujiza mengi aliyokuja nayo.
 
Miujiza ya Nabii Isa (AS):
 
Nabii Isa (AS) au Yesu alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbali mbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa ni kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuh na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbali mbali
 
Salim Elhaj
Anonymous user