Isa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 17:
Wakristo au Manasara wanahitalifiana katika itikadi yao kuhusu Nabii Isa (AS), kwani kuna wanaomchukulia kuwa ni mtoto wa Mungu, na wengine wanaomuitakidi kuwa ni Mungu, na kuna kundi linalomchukulia kuwa ni Mtume au Nabii. Makundi haya yalitafautiana baada ya kuondoka Nabii Isa (AS) ulimwenguni na kuwawacha wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada yake, mbali na wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walikuja na fikra na mawazo mengine kuhusu Isa au Yesu kama anavyojulikana na Wakristo, na baada ya muda waligawanyika makundi mbali mbali, wakiwa wengine wanamuamini kuwa ni Mtume na Nabii kama alivyowafundisha na wengine wakawa wanamuamini kama ni mtoto wa Mungu au Mungu kwa sababu ya miujiza mengi aliyokuja nayo.
 
'''Miujiza ya Nabii Isa (AS):'''
 
Nabii Isa (AS) au Yesu alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbali mbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa ni kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuh na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbali mbali. Baadhi ya miujiza ya Nabii Isa (AS)ni kuumba ndege kutokana na udongo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kuponyesha vipofu wakaweza kuona, na kuwaondoshea ukoma wale wenye ukoma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kuhuisha mtu aliyekufa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kuwateremshia wafuasi wake chakula kutoka mbinguni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ili iwe ni dalili kwao wote.
 
'''Kitabu cha Nabii Isa'''
 
Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya uwongozi na sharia na hekima kwa wafuasi wao. Katika vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii mbali mbali ni Taurati kwa Nabii Musa, Zaburi kwa Nabii Daudi, Injili kwa Nabii Isa, na Qurani kwa Nabii Muhammad. Kitabu cha Nabii Isa - Injili - kiliteremshiwa Mayahudi ambao ndio wafuasi hasa wa Nabii Isa, kama alivyoeleza katika Biblia kuwa sikuletwa isipokuwa kwa wana kondoo waliopotea wa nyumba ya Israili, na haya yamethibitishwa ndani ya Qurani wakati aliposema kuwa:
 
'''''Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi!'''''
 
Salim Elhaj