Tofauti kati ya marekesbisho "Isa"

1,264 bytes added ,  miaka 16 iliyopita
Nabii Isa (AS) - Kuzaliwa kwake - Ujumbe wake - Itikadi ya Kikristo kuhusu Isa - Miujiza ya Nabii Isa - Kitabu cha Nabii Isa - Kuletwa tena kwa Nabii Isa
(Nabii Isa (AS) - Kuzaliwa kwake - Ujumbe wake - Itikadi ya Kikristo kuhusu Isa - Miujiza ya Nabii Isa - Kitabu cha Nabii Isa - Kuletwa tena kwa Nabii Isa)
'''Nabii Isa (AS)'''
 
Nabii Isa (AS) ni Mtume anayeaminiwa na Waislamu kama mmojawapo wa Mitume mitukufu wa Mwenyezi Mungu walioletwa kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu duniani, naye ni miongoni mwa Mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahmilivu wao mkubwa. Nao ni Manabii Nuhu na Ibrahim na Musa na Isa na Muhammad (amani na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao). Yeye ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili.
 
Nabii Isa (AS) ni mmojawapo wa 124,000 wa mfululizo wa Mitume na Manabii wa Mwenyezi walioletwa ulimwenguni kuwaletea ujumbe wanadamu wa Mwenyezi Mungu kuhusu upweke na umoja wake, na kumuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani. Watume na Manabii hawa wameletwa katika zama mbali mbali na kwa watu, kaumu na umma mbali mbali, na mfululizo huu ulianza na Adam (AS) baba wa wanadamu wote hadi Mtume Muhammad (SAW) akiwa ndiye wa mwisho katika Manabii na Mitume.
'''Kuzaliwa kwake'''
 
Nabii Isa (AS) alizaliwa na bibi Maryam kimiujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimleteaalimtuma Jibrili (AS) kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa (AS), alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwengine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mamake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba. Huu ni mfano mmoja katika mifano minne aliyotuonyesha Mwenyezi Mungu ya uumbaji, kwani Mwenyezi Mungu alimuumba Adam (AS) bila ya baba wala mama, na akamuumba Hawa bila ya mama, na akamuumba Isa bila ya baba, na akaumba wanadamu wote waliobakia kutokana na baba na mama.
 
'''Ujumbe wake'''
 
Nabii Isa (AS) aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki, na ujumbe huu ndio ujumbe uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kupa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) ambao ndio ulikuwa wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote. Alipokuja alitabiri kuwa atakuja baada yake Mtume ambaye atawafundisha wanadamu ukweli wote na kuwaongoza kwenye haki na kuwaeleza kila wanalolihitajia katika maisha yao.
 
'''Itikadi ya Kikristo kuhusu Isa (AS)'''
 
'''''Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi!'''''
 
'''Kuletwa tena kwa Nabii Isa (AS)'''
 
Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa au Yesu atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake aliyoiwacha baada ya kuondoka kwenda kwa Mola wake, na haya yanaelezwa katika vitabu vya dini vya Kiislamu na vya Kikristo, lakini wanahitalifiana kuhusu namna na njia aliyoondokea ulimwenguni. Waislamu wanasema kuwa Isa (AS) alichukuliwa na Mola wake na kupandishwa kwake mbinguni baada ya Mayahudi kutaka kumuua, na kwa hivyo hawakuweza kumuua wala kumsulubu. Baadhi ya Wakristo kwa upande mwengine, wanaamini kuwa aliwahi kusulubiwa na kuzikwa kisha akafufuka siku ya tatu yake. Muhimu hapa ni kujua kuwa Isa au Yesu atarudi tena duniani kukamilisha kazi yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu.
 
Salim Elhaj
Anonymous user