Bara : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Bara (Kontinenti) - Mabara ya Ulimwengu - Eneo la dunia - Maeneo ya Mabara haya
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:28, 28 Machi 2005

Bara (Kontinenti)

Kontinenti au Bara ni sehemu kubwa ya ardhi iliyochomoza juu ya bahari, ambayo kikawaida hukaliwa na watu na kuwa juu yake milima na mimea na wanyama na kila aina ya viumbe. Sehemu hii ya ardhi ndio inayojulikana kama bara, na sehemu nyengine ya ardhi ni ile iliyoko chini ya bahari. Yako katika ulimwengu mabara saba, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo.

1- Bara la Afrika 2- Bara la Asia 3- Bara la Amerika ya Kaskazini 4- Bara la Amerika ya Kusini 5- Bara la Antaktika 6- Bara la Australia 7- Bara la Uropa

Mabara ya Ulimwengu

Kuna katika ulimwengu wetu huu, mabara saba (7): Asia, Afrika, Amerika ya kaskazini, Amerika ya kusini, Antaktika, Australia na Ulaya (Uropa). Eneo la mabara haya ni kama ifuatavyo, kuanzia na kubwa kabisa hadi dogo kabisa.

1- Bara la Asia lina eneo la 44,579,000 kilomita mraba. 2- Bara la Afrika lina eneo la 30,065,000 kilomita mraba. 3- Bara la Amerika ya kaskazini lina eneo la 24,256,000 kilomita mraba. 4- Bara la Amerika ya kusini lina eneo la 17,819,000 kilomita mraba. 5- Bara la Antaktika lina eneo la 13,209,000 kilomita mraba. 6- Bara la Australia lina eneo la 7,687,000 kilomita mraba. 7- Bara la Uropa au Ulaya lina eneo la 9,938,000 kilomita mraba.

Eneo la dunia

Eneo la ardhi yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu.

Maeneo ya Mabara haya

1- Bara la Asia lina nchi huru 44. 2- Bara la Afrika lina nchi huru 53. 3- Bara la Amerika ya kaskazini lina nchi huru 23. 4- Bara la Amerika ya kusini lina nchi huru 12. 5- Bara la Antaktika halina nchi huru hata moja ijapokuwa nchi kama 7 zinadai kumiliki sehemu fulani za bara hili. 6- Bara la Australia au Oshania lina nchi huru 14. 7- Bara la Uropa au Ulaya lina nchi huru 46.

Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi.

Salim Elhaj