Vita kati ya Irak na Uajemi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 4:
Vita ilianza kwa mashambulio ya Irak dhidi ya Uajemi. [[Dikteta]] [[Saddam Hussein]] wa Irak alitaka kutumia nafasi ya kudhoofishwa kwa jeshi la Uajemi baada ya mapinduzi ya mwaka 1979. Mwaka ule serikali ya [[shah]] ya Uajemi ilipinduliwa na harakati iliyoongozwa na kiongozi Mwislamu [[Ruhollah Khomeini]] na maafisa wengi wa jeshi la shah ama waliuawa au kukimbia nchi. Saddam Hussein alilenga kushika utawala juu ya [[Shat al Arab]] ambayo ni mdomo wa mito Frati na Hidekeli kwenye ghuba ambako mizigo ya [[mafuta ya petroli]] ya Irak inapaswa kupita ikiuzwa nje. Alilenga pia kutwaa sehemu za Uajemi zilizokuwa na wasemaji wa lugha ya Kiarabu na sehemu hizi zinaitwa [[Khuzistan]]; Saddam alidai ya kwamba ilikuwa eneo la Kihistoria ya Irak iliyokamatwa na Uajemi.
 
Mwanzoni Wairaki walifaulu kuteka maeneo karibu na mpakani upande wa Uajemi lakini serikali mpya ya Kiislamu iliweza kutuma wanamigambo hasa vijana wengi ambao walikuwa tayari kufa hata kama hawakufundishwa kazi ya askari. Mtindo huu ulirudisha Wairaki nyuma lakini likuwaulikuwa pia sababu ya kwamba Waajemi wengi walikufa kushinda Wairaki. Ila tu Uajemi ni nchi yenye watu wengi zaidi na Waajemi wengi walikuwa tayari kwa kifo kwa sababu waliona ya kwamba nchi yao ilishambuliwa. Viongozi wa kidini walitangaza ya kwamba ilikuwa wajibu wa kidini kushika silaha.
 
Nchi za nje kama Marekani zilihofia mapindizi ya Kiislamu zikasaidia Irak kwa silaha na habari kama picha kutoka vyombo vya angani. Vita hii ilikuwa maarufu kwa sababu Irak ilitumia silaha marufuku kama gesi ya sumu.
 
Vita iliendelea ingawa [[Umoja wa mataifa]] ilisihi pande zote mbili kumaliza mauaji. Mwishowe walipatana kusimamisha mapigano na kurudi kwa mipaka ya kimataifa kwa sababu ya uchovu na uharibifu mkubwa kwenye pande zote mbili.
 
 
<gallery>
Image:Chemical weapon1.jpg|Wanajeshi wa Uajemi wakivaa kinga dhidi ya silaha za sumu
Image:Yazd3.JPG|Makaburi wa wafu wa vita mjini [[Yazd]] (Uajemi)
Image:Capture in Khorramshahr.jpg|Wanajeshi wa Iraki waliojisalimisha mjini [[Khoramshahr]]
</gallery>
 
==Marejeo ya Nje==