Yuda Tadei : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: right|200px|thumb|Sanamu yake katika [[Kanisa Kuu la Roma]] '''Yuda Tadei''' ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, am...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 23:10, 7 Februari 2009

Yuda Tadei ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambalo Injili zinajitahidi kumtofautisha na Yuda Iskariote, msaliti wa Yesu.

Sanamu yake katika Kanisa Kuu la Roma

Habari zake za hakika zinategemea Agano Jipya ambamo anatajwa katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama msingi wa taifa jipya la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.

Injili ya Yohane tu inaripoti neno lake moja, katika simulizi la karamu ya mwisho, alipomuuliza Yesu imekuwaje atajifunua kwao lakini si kwa ulimwengu (14:22). Yesu alimjibu kwamba yeyote anayempenda atashika neno lake, na Baba atampenda na kufanya maskani yake kwake pamoja na Mwana.

Anafikiriwa na wengi kuwa mwandishi wa Waraka wa Yuda, lakini hakuna hakika kwa sababu jina hilo la babu wa Wayahudi wote lilikuwa la kawaida mno.