Kano (jimbo) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
(Hakuna tofauti)

Pitio la 15:07, 17 Oktoba 2006

Kano ni jimbo la kujitawala katika kaskazini ya Nigeria. Mji mkuu ni Kano mjini.

Jimbo la Kano limepakana na majimbo ya Katsina, Jigawa, Kaduna na Bauchi. Jimbo lilianzishwa tar. 27 Mei 1967. Gavana wa kwanza alikuwa Abdu Bako kuanzia 1967 hadi Julai 1975. Ibrahim Shekarau amekuwa gavana tangu 29 Mei 2003.

Eneo la jimbo ni 20,131 km², idadi ya wakazi 10,077,638 (mwaka 2005). Msongamano wa watu hufikia wakazi 501 kwa kilimita ya mraba.

Jimbo lina maeneo ya utawala 44 ("Local Government Areas"). Haya ni: Ajingi, Albasu, Bagwai, Bebeji, Bichi, Bunkere, Dala, Dambatta, Dawakin-Kudu, Dawakin-Tofa, Doguwa, Fagge, Gabasawa, Garko, Garum-Mallam, Gaya, Gazewa, Gwale, Gwarzo, Kabo, Kano Municipal, Karaye, Kibiya, Kiru, Kumbotso, Kunchi, Kura, Madobi, Makoda, Minjibir, Nassarawa, Rano, Rimin-Gado, Rogo, Shanono, Sumaila, Takai, Tarauni, Tofa, Tsanyawa, Tudun-Wada, Ungongo, Warawa na Wudil.

Kano ni kitovu cha biashara na uzalishaji mali nchini. Asilimia ya umwagiliaji wa mashamba inazidi majimbo yote na kuruhusu kilimo mwaka wote.


Kategorie:Majimbo ya Nigeria