Tofauti kati ya marekesbisho "Wilaya ya Mkuranga"

1,376 bytes added ,  miaka 12 iliyopita
no edit summary
'''Wilaya ya Mkuranga''' ni wilaya moja ya [[Mkoa wa Pwani]]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 187,428 [http://www.tanzania.go.tz/census/census/districts/mkuranga.htm].
 
==Eneo==
Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1995 kutokana na maeneo ya [[wilaya ya Kisarawe]]. Eneo lake ni 2,432 [[km²]] na kuna pwani la Bahari Hindi lenye urefu wa kilomita 90. Vijiji saba viko kando la pwani ni hungubweni, Mpafu, Kerekese, [[Kisiju]] Pwani, Mdimni, Magawa na Kifumangao. Vijiji vya Boza, Kuruti, [[Kwale (Kisiju)|Kwale]] na Koma viko kwenye visiwa vidogo baharini si mbali na pwani.
 
Kuna misitu ya mikoko na wanyama walio hatarini ya kuangamizwa bado wana hifadhi hapa.
 
 
==Wakazi==
Wenyeji ni hasa [[Wazaramo]], [[Wandengereko]], [[Wamatumbi]] and [[Wamakonde]].
 
Wakazi wa wilaya hukalia kata 15 zenye vijiji 101. Walio wengi (zaidi ya 90%) hudumisha maisha yao kwa njia ya kilimo hasa kilimo cha [[muhogo]], [[mpunga]] na [[maharagwe]]. Mazao ya biashara ni [[korosho]], [[nazi]], [[mananasi]] na [[machungwa]]. Eneo hili ilikuwa kitovu cha kilimo cha korosho Tanzania takriban hektari 35,000 ilitumiwa kwa zao hili lakini tangu miaka ya 70 kilimo kilianza kupungua.
 
Wakazi wa vijiji vya pwani wanavua samaki.
 
Watu walio wengi ni maskini na utafiti wa mwaka 2005 ulionyesha kuwa familia ya wastani yenye watu 4.5 ilikuwa na pato la TSh 600,000 kwa mwaka (sawa na [[dola za Marekani]] 600) yaani chini ya dola 150 kwa mwaka kwa kila mtu.
 
 
 
==Marejeo ya Nje==
*[http://www.crc.uri.edu/download/Mkuranga_baseline.pdf Mkuranga Governance Baseline (USAID)]
 
{{Kata za Wilaya ya Mkuranga}}
Anonymous user