Wadominiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:Blason LBP.svg|right|thumb|Lebo ya shirika]]
[[Image:SaintDominic.jpg|right|thumb|[[Dominiko wa Guzmán]], [[mwanzilishi]] wa Shirika la Ndugu Wahubiri]]
[[Image:San Domenico11.jpg|thumb|right|225px|Mdominiko katika [[kanzu]] rasmi ya shirika]]
'''Wadominiko''' ni jina fupi linalotumka kuhusu wafuasi wote wa [[Dominiko wa Guzmán]] ([[1170]]-[[1221]]), hasa wa '''Shirika la Ndugu Wahubiri''' alilolianzisha, mojawapo kati ya mashirika ya [[utawa|kitawa]] ya [[Kanisa Katoliki]], aina ya [[Ombaomba]]. Ufupisho wa jina la shirika ni '''O.P.'''
 
==Historia==
Shirika lilianzishwa na [[Dominiko wa Guzmán]], [[mkanoni]] wa [[jimbo]] la [[Burgo de Osma-Ciudad de Osma]]: mwaka [[1203]] aliongozana na [[askofu]] wake [[Diego wa Acevedo]] katika safari ya kibalozi kwa niaba ya [[mfalme]] [[Alfonso VIII wa Castilia]] kwa mfalme [[Valdemaro II wa Denmark]]. Wakati wa kurudi, wakipitia mkoa wa [[Langadoque]] ([[Ufaransa]] Kusini), waling'amua [[uzushi]] wa [[Wakatari]] ulivyoenea naye akaamua kuungana na mabalozi wa [[Papa Inosenti III]] katika jitihada za kurudisha watu hao katika [[Kanisa Katoliki]].
 
Akikusanya kundi dogo la wasichana walioacha Ukatari, maka [[1207]] alianzisha huko Notre-Dame-de-Prouille, karibu [[Fanjeaux]], [[monasteri]] ya kike ambayo ikawa kitovu cha kazi yake ya kitume.
 
Dominiko aliendelea kuwahubiri kwa amani Wakatari hata baada ya [[balozi]] wa [[Papa]] [[Petro wa Castelnau]] kuuawa ([[1208]]), akikataa kujiunga na [[vita vya msalaba]] vilivyotangazwa dhidi ya Wakatari.
 
Kwa msaada wa askofu wa [[Tolosa]] Folco, mwaka [[1215]] alikusanya wenzi kadhaa wenye nya ya kuhubiri kama yeye akawaingiza katika [[utawa|maisha ya kitawa]]: shirika hilo lilipata kwanza kibali fulani cha [[Papa Inosenti III]] halafu kibali rasmi cha mwandamizi wake, [[Papa Onori III]], tarehe [[22 Desemba]] [[1216]].
 
Baada ya hapo Shirika la Ndugu Wahubiri lilienea kati [[Ulaya]] nzima, hasa katika miji ambapo vilikuwa vinaanza [[chuo kikuu|vyuo vikuu]], kama vile vya [[Bologna]] na [[Paris]], vilivyosaidiwa sana na Wadominiko kupata ustawi.
 
Kwa agizo la [[Mtaguso IV wa Laterano]] ndugu hao walipaswa kujichagulia [[kanuni]] iliyowahi kukubaliwa na [[Kanisa]], wakaamua kushika ile ya [[Agostino wa Hippo]], wakiiongezea [[katiba]] ya kwao, maarufu hasa kwa kutumia kiasi fulani cha [[demokrasia]], ambayo ilitumiwa kama mwongozo kwa nyingine hata za kiserikali.
 
==Karama==
Ni hasa ile ya kuhubiri, ambayo wakati ule ilikuwa ya nadra, kutokana na hali ya elimu hata kati ya ma[[kasisi]]. Utume huo, uliokubaliwa na Papa kwa wanashirika wote, ukawa msaada mkubwa kwa Kanisa pia kwa sababu uliendana na maisha ya [[ufukara wa Kiinjili]].
 
Mambo muhimu ya shirika ni:
*Kuhubiri [[Injili]]
*Kuishi kijumuia
*Kuadhimisha [[liturujia]]
*Kushika taratibu za kitawa
*Kusoma
 
 
==Takwimu==