Kislovakia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with '{| cellpadding="2" cellspacing="0" style="vertical-align:top;float:right;width:300px;border:1px solid #ccc;margin-left:1em;" ! colspan="2" style="background-color:#A9BEC7;font-si…'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:49, 3 Aprili 2009

Kislovakia ni lugha rasmi inayoongelewa nchini Slovakia, nchi iliyopo Mashariki mwa Ulaya. Ni moja kati ya Lugha za Kislavoni, mkusanyiko wa lugha unajumlisha Kirusi, Kipoland na lugha nyingine kadhaa za Mashariki ya Ulaya.

Kislovakia
Kinamzungumzwa nchini: Slovakia, Ucheki, Vojvodina (kwa 2,79% ya watu) Marekani, Kanada, Australia, Hungaria, Croatia na Ukraine
Wazungumzaji: Milioini 6
Lugha rasmi:
Nchi: Slovakia
Uainishaji wa kiisimu:
Lugha za Kihindi-Kiulaya
   Lugha za Kislavoni
      Kislavoni cha Magharibi
         Kundi la Lugha za Kicheki-Slovakia
            Slovak language

Lugha hii inafanana kabisa na Kicheki, na Wacheki na Wasovakia wanaweza kuelewana vizuri kabisa wakiwa wanazungumza lugha zao. Kipoland na Kisorbia kina fanana kabisa. Kislovakia kinazungumzwa nchini Slovakia na zaidi ya watu milioni 5.

Matamshi

Kislovakia kinaandikwa kutumia alfabeti za Kilatini, lakini kuna viji herufi fulani ambavyo viji harama maalum (vinaitwa “diacritics”).

Herufi č, š, ž and dž zina sauti kama ile ya Kiingereza katika chin, shin, vision na juice.

Herufi ď, ľ, ň, and ť huitwa “konsonanti nyepesi”. Hutamkwa kwa kukata ulimi juu kabisa ya mdomo.

C, dz na j nazo pia ni nyepesi. C ipo kama ts katika bats, dz ipo kama ds katika rods, na j ipo kama y katika yes.

Alama zake katika voweli huonyesha kwamba voweli hutamkwa kwa urefu zaidi: á, é, í, ó, ý ú. Voweli ndefu haifuati katika silabi inayofuata kwa kutumia voweli fupi.

Ile ô ipo kama Kiingereza wombat, na ä ni sawa na herufi e.

Ch ipo kama ch katika Kiscoti loch. V ni zaidi ya Kiingereza w.

Herufi b, d, ď, dz, dž, g, h, z, ž hazisikiki pale wakiwa wanamalizia (kwa mfano: 'd' itasikika kama 't').

Kistress ndiyo inayotumika kuanzishia silabi ya neno. Hii ni tofauti kabisa na Kirusi, kwa mfano, wapi Kistress kinaweza kikawa.

Kama jinsi ilivyo katika lugha zingine za Kislavoni, Kislovakia ni vigumu kwa wazungumzaji wa Kiingereza kuweza kutamka. Hii hasa kwa sababu maneno kadhaa yameambatanisha konsonanti nyingi kuwa pamoja. Katika sentensi: “Strč prst skrz krk!” hakuna hata voweli moja (ina maana: “Zungusha vidole kwenye shingo yako!”)!