Wapangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
dNo edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Wapangwa''' ni kabila kutoka [[Milima Livingstone]] karibu na pwani ya mashariki ya [[Ziwa Nyasa]], [[wilaya ya Ludewa]], [[Mkoa wa Iringa]], kusini ya nchi ya [[Tanzania]]. Mwaka 2002 idadi ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 95,000.
 
Chakula chao ni [[ugali]] wa [[mahindi]], [[ulezi]] na [[mtama]] kidogo. Kitoweo cha vyakula hivyo ni [[maharage]], samaki, [[nyama]] na jamii ya mboga mboga. Kinywaji chao ni pombe (ukhimbi) yaani kangala, komoni, [[ulanzi]] ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi.
 
Hulima mazao mbalimbali katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito. Ni wafugaji wa [[ng'ombe]], [[mbuzi]], [[kondoo]] na [[nguruwe]] (kitimoto). Pia hulima mazao ya biashara kama [[kahawa]], [[chai]], [[pareto]], [[mahindi]]. Kabila hili pia hupata matunda ya asili kama vile; masada, savula, makuhu, mahofita, minhingi, vudong'o na nisongwa.