Karama : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with ''''Karama''' ni zawadi inayotokana na ukarimu wa Mungu kwa viumbe wake. Neno hilo limekuwa likitumika sana katika Kanisa kuanzia Pentekoste na katika Agano Jipya,…'
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Karama''' ni zawadi inayotokana na ukarimu wa [[Mungu]] kwa viumbe wake. Neno la [[Kigiriki]] χάρισμα ("kharisma") linatokana na χάρις, "kháris" (neema). Neno hilo limekuwa likitumika sana katika [[Kanisa]] kuanzia [[Pentekoste]] na katika [[Agano Jipya]], hasa katika barua za [[Mtume Paulo]], kwa msisitizo kuwa karama zote zinamtegemea [[Roho Mtakatifu]].
 
Karama si zile za kushangaza tu, tena zile muhimu zaidi si hizo, bali zile zinazojenga zaidi Kanisa, kama zile za uongozi: “Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha” (1Kor 12:28). “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha” (Rom 12:6-8).
Mstari 8:
 
Karama za kushangaza zina hatari mbalimbali, hasa zikitiwa maanani mno. Hapo ni rahisi zilete [[majivuno]], [[kijicho]] na ma[[farakano]]. “Ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je, si watu wa tabia ya mwili ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?... Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki... Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 3:3; 4:8; 10:12). Katika mambo yasiyothibitika ni rahisi kudanganyika kuwa yametoka kwa Mungu, kumbe sivyo. Kisha kudanganyika ni vigumu kuachana nayo hata yakiwa na madhara kwa mhusika au kwa Kanisa. “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” (1Yoh 4:1).
[[Category:Biblia]]
[[Category:Teolojia]]
[[Category:Ukristo]]
 
[[ar:كاريزما]]
[[bg:Харизма (религия)]]
[[ca:Carisma]]
[[cs:Charisma]]
[[da:Karisma]]
[[de:Charisma]]
[[en:Charisma]]
[[es:Carisma]]
[[fa:فرهمندی]]
[[fi:Karisma]]
[[fr:Charisme (psychologie)]]
[[he:כריזמה]]
[[hr:Karizma]]
[[it:Carisma (cristianesimo)]]
[[ja:カリスマ]]
[[ko:카리스마]]
[[lt:Charizma]]
[[mk:Харизма]]
[[nl:Charisma (karakter)]]
[[no:Karisma]]
[[pl:Charyzma]]
[[pt:Carisma]]
[[ro:Carismă]]
[[ru:Харизма]]
[[sk:Charizma (sociológia)]]
[[sr:Харизма]]
[[sv:Karisma]]
[[tr:Karizma]]
[[uk:Харизма]]