Mtawa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with ''''Mtawa''' ni mtu anayejitenga na ulimwengu ili kuishi maisha maadilifu. Katika dini mbalimbali, mfano mmojawapo ni ule wa wamonaki. Lakini katika Ukristo, [[histor…'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:04, 2 Mei 2009

Mtawa ni mtu anayejitenga na ulimwengu ili kuishi maisha maadilifu.

Katika dini mbalimbali, mfano mmojawapo ni ule wa wamonaki. Lakini katika Ukristo, historia ya utawa ilitokeza aina mbalimbali.

Katika Kanisa Katoliki, ni mwamini yeyote aliyejiweka wakfu hasa kwa kushika useja mtakatifu, na kwa kawaida pia ufukara na utiifu.

Mara nyingi watawa wanaunda mashirika yenye karama moja inayofafanuliwa na kuratibiwa katika kanuni na katiba maalumu.

Mtawa anaweza kuwa mwanamume au mwanamke, mwenye daraja takatifu au la.