Bradha : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with 'thumb|right|230px|Bradha [[Wafransisko|Mfransisko]] '''Bradha''' au '''bruda''' (yaani ndugu wa kiume) ni neno la mkopo linalotumika katika [[lug…'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 16:39, 7 Mei 2009

Bradha au bruda (yaani ndugu wa kiume) ni neno la mkopo linalotumika katika lugha ya Kiswahili hasa kumaanisha mtawa wa kiume, wakati yule wa kike anaitwa sista.

Bradha Mfransisko

Lakini katika mashirika mengi, linatumika hasa kumaanisha mtawa wa kiume asiye kasisi. Ingawa watawa wengi wa kiume ni mapadri pia, si lazima iwe hivyo.

Hali ya kuwekwa wakfu kwa kuahidi utekelezaji wa mashauri ya Kiinjili (useja mtakatifu, ufukara, utiifu)) inajitosheleza kama ilivyo kwa masista. Kwa kuwa lengo la utawa si kuongoza Kanisa kwa mamlaka inayotokana na daraja takatifu au kutoa huduma za kipadri, bali ni kulenga utakatifu, yaani upendo kamili.