Kitubio : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 7:
 
[[Image:SantCompostela25.jpg|thumb|230px|Masanduku ya Kitubio katika [[Kanisa kuu]] la [[Santiago wa Compostela]] ([[Hispania]])]]
 
==Msingi wa [[teolojia]] yake katika [[Biblia]]==
 
Kadiri ya imani hiyo, tunaweza kuona ina msingi gani katika [[ufunuo]], hasa [[Agano Jipya]]. Ufafanuzi wake wa kichungaji unaweza kuwa kama ifuatavyo.
 
Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa njia ya Mwanae. [[Yesu]] mfufuka aliwaonyesha [[Mitume wa Yesu|Mitume]] alama ya mateso mwilini mwake, “akawavuvia, akawaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23). Katika [[Kanisa]] tunafurahi kupewa msamaha wa dhambi kila tunapohitaji, mradi tutubu. Kwa njia ya mwandamizi wa Mitume, Yesu anatuambia, “Umesamehewa dhambi zako... Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani” (Lk 7:48,50). Si dhana wala hisia tu, bali ni neno la hakika tunalolipokea kwa masikio yetu.
 
Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi zote, kwa sababu [[upendo]] mtiifu wa Mwanae aliyejitoa kuwa [[sadaka]] ya [[wokovu]] wetu unampendeza kuliko dhambi zote zinavyomchukiza. Ila hatuwezi kusamehewa dhambi ya kukataa [[neema]] ambayo [[Roho Mtakatifu]] anatusukuma tuamini na kutubu, kwa sababu pasipo [[imani]] na [[toba]] hapana [[msamaha]]. “Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa” (Math 12:31). “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure” (2Kor 6:1).
 
Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa sababu amependa washiriki katika kazi zake. Ametuumba kwa njia ya wazazi na kutulea na kutusaidia kwa njia ya wengine pia. Hasa ametuokoa kwa njia ya Yesu, ambaye yupo nasi sikuzote katika Mwili wake, yaani Kanisa, na katika wale walioshirikishwa [[mamlaka]] ya Mitume. “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo: mpatanishwe na Mungu” (2Kor 5:18-20).
 
Hivyo, tumuendee [[upadri|padri]] ili kuondolewa dhambi tulizotenda baada ya ubatizo, kwa kuwa hatuwezi kupokea msamaha tukikataa masharti yake, na Mungu ametupangia watu ambao watuondolee kwa niaba yake. “Watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa [[Yohane Mbatizaji|Yohane]]. Lakini, [[Mafarisayo]] na wanasheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye” (Lk 7:29-30). Yesu mwenyewe alikubali kubatizwa na Yohane ili atimize mpango wa Baba. “Yohane alitaka kumzuia, akisema, ‘Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?’ Yesu akajibu akamwambia, ‘Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Math 3:14-15). Je, sisi tukatae kumkimbilia padri wa Mungu ili kupokea [[huruma]] yake tunayoihitaji kuliko hewa?
 
Tumuungamie padri dhambi zetu ili aweze kutushauri na kuamua kama tuko tayari kuondolewa. Tumweleze kwa [[unyofu]] makosa yote tuliyoyafanya na nia tuliyonayo ya kuyafidia na kutoyarudia. “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo, wala neno lake halimo mwetu” (1Yoh 1:8-10). Tukumbuke tulivyo viungo vya Mwili mmoja, hivi kwamba dhambi zetu zimewadhuru wenzetu. “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana, mpate kuponywa” (Yak 5:16). Kutokuwa tayari kufanya hivyo walau sirini kwa padri ni dalili ya [[kiburi]] na ya kutotubu.
 
Hata padri akiwa mkosefu, anaweza kutuondolea dhambi kwa niaba ya Mungu aliyempa mamlaka hiyo. Hatusamehewi na [[utakatifu]] wa padri, bali na huruma ya Baba kwa njia yake. Yeye anamtumia padri yeyote ili kuturahisishia kazi, tusihitaji kuchunguza kwanza ubora wa maisha yake, wala kwenda mbali tukampate mmoja asiye na dhambi. Tungefanyeje kuhakikisha ni mtakatifu, wakati hatuwezi kusoma moyo wake? Ingekuwa hivi, tusingepata kamwe hakika ya kusamehewa. Kumbe inatutosha kujua ni padri, kwamba Mungu amempa mamlaka ya kusamehe dhambi, kama Yesu alivyowapa Mitume siku tatu baada ya kumkimbia na hata kumkana. Kila padri anaweza kukiri, “Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa: ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi, ambao wa kwanza wao ni mimi” (1Tim 1:15). Amri ya kusamehe dhambi wamepewa watu, si [[malaika]]. “Tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu” (2Kor 4:7).
 
Nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo, lakini ni vigumu zaidi, kwa sababu hatupati msaada wa sakramenti hiyo maalumu. Pamoja na nia ya kumuungamia padri mapema tunahitaji neema ya kutubu kikamilifu, si kwa kuhofia [[adhabu]], bali kwa kumpenda Mungu tuliyemchukiza. “Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana” (Lk 7:47).
 
 
[[Category:Liturujia]]