Mpako wa wagonjwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Ondoa: hu:Betegek kenete; cosmetic changes
No edit summary
Mstari 2:
[[Picha:Extreme Unction Rogier Van der Weyden.jpg|thumb|left|300px| Sehemu ya mchoro ''Sakramenti Saba'' ([[1445]]) wa [[Roger van der Weyden]] ikionyesha ''Mpako wa Wagonjwa''.]]
 
'''Mpako wa wagonjwa''' ni [[ibada]] maalumu kwa ajili ya wagonjwa inayotumiwa na [[Ukristo|Wakristo]] wa [[madhehebu]] mbalimbali kufuatana na desturi ya [[Mitume wa Yesu]] na agizo la [[Waraka wa Yakobo|Barua ya Yakobo]].
 
Kwa [[Kanisa Katoliki]], [[Waorthodoksi]] na madhehebu mengine machache ni [[sakramenti]] iliyowekwa na [[Yesu Kristo]], ingawa [[Injili]] haisemi.
 
Pamoja na [[Kitubio]] ni kati ya sakramenti mbili za uponyaji, zinazolenga kumrudishia Mkristo afya ya [[roho]] na [[mwili]], iliyoathiriwa na [[dhambi]] na [[ugonjwa]].
 
Kadiri ya [[imani]] hiyo, Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na [[Yesu]], kama sakramenti zote. [[Biblia|Maandiko]] yanasimulia [[huruma]] yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa “kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina” (Math 10:1). Nao “wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza” (Mk 6:13). “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa” (Yak 5:14-15).
 
[[Mafuta]] ya wagonjwa yanamaanisha lengo la kuwaponya na kuwarudishia [[nguvu]] na [[uzuri]]. Kama kawaida, maneno yanaweka wazi zaidi kuwa lengo si kuponya [[mwili]] tu, bali hasa [[roho]] kwa kuitia [[msamaha]] na [[faraja]] katika mateso ambayo huenda yakaendelea. Kwa kuwa [[Mungu]] haponyi mwili kila mara, isipokuwa kwa faida na [[wokovu]] wa [[mgonjwa]] na wa wengine. Kama ndiyo mapenzi yake, kila mmoja ajifunze kufaidika vilevile na [[ugonjwa]]: “Makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, ‘Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu’. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu” (2Kor 12:7-9). “Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake” (Kol 1:24).
 
 
== Viungo vya nje ==