Daraja takatifu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: zh:聖秩聖事
No edit summary
Mstari 1:
{{Sakramenti}}
 
Katika [[Ukristo]] zinaitwa '''daraja takatifu''' vyeo vya [[askofu]], [[kasisi]] na [[shemasi]] vinaitwa pengine '''daraja takatifu'''.
 
Katika [[Kanisa Katoliki]] na ya [[Waorthodoksi]] ngazi hizo tatu zinaunda kwa pamoja mojawapo ya [[sakramenti]] saba ambazo [[Yesu Kristo]] alizianzisha na kulikabidhi [[Kanisa]] lake.
Mstari 13:
==Ibada ilivyo==
 
Tangu zamani za [[Mitume wa Yesu]] mamlaka inashirikishwa kwa tendo la kumwekea mtu mikono kichwani, kufuatana na mfano wa [[Musa]] kwa [[Yoshua]] katika [[Agano la Kale]].
 
Tendo hilo linafuatana na sala maalumu ambayo, katika kumuomba [[Roho Mtakatifu]] amshukie mhusika, inaweka wazi daraja gani inatolewa.
Mstari 24:
==Anayeweza kupewa==
 
Ni imani ya [[Kanisa Katoliki]], ya makanisa ya [[Waorthodoksi]] na ya [[madhehebu]] mengine kadhaa kwamba daraja zinaweza kutolewa kwa wanaume tu, kwa sababu [[Yesu]] aliteua watu wa jinsia hiyo tu awape mamlaka yake ambayo inashirikishwa kwa daraja hizo, na kwa sababu ndiyo [[mapokeo]] ya Kanisa tangu mwanzo.
 
Waprotestanti wanazidi kukubali wanawake katika nafasi zote za uongozi, wakisisitiza usawa wa wafuasi wa Yesu.
Mstari 32:
==Hali ya kudumu==
 
Sawa wa sakramenti za [[Ubatizo]] na [[Kipaimara]], katika [[imani]] ya Wakatoliki daraja takatifu zinamtia mwamini ''[[alama isiyofutika]]'' ya ki[[kuhani]] aweze kumtolea [[Mungu]] ibada katika [[liturujia]] na katika maisha yake yote.
 
Kwa maana hiyo daraja inadumu ndani ya mtu hata akiacha kutoa huduma au kuasi kabisa.
 
==Misingi ya imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi katika [[Biblia]]==
 
Kadiri ya [[imani]] hiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na [[Kanisa]] kwa sababu kazi ya [[wokovu]] haimtegemei [[binadamu]], bali [[Mungu]]. “Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” (Eb 5:4-5), bali alisisitiza alivyopewa na [[Baba]] uwezo wa kutuokoa. “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake” (Yoh 3:35). “Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yoh 17:2). Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18-20). Mpaka [[mwisho wa dunia]] uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa [[mamlaka]]. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.
 
Wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo. “Amin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipeleka” (Yoh 13:20). “Jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu” (Gal 4:14). “Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii” (Tito 3:1). Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia. “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha” (1Tim 5:17).
 
Wenye daraja wanaweza wakatenda [[dhambi]] kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. [[Yesu]] alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso. “Je, mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?” (Yoh 6:70). “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao, na kuniacha mimi peke yangu” (Yoh 16:32). [[Mtume Paulo]] alionya mapadri, “Katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Mdo 20:30).
 
Kadiri ya [[Injili]] ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa hasa kusali. “Mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake” (Math 9:38). Halafu yanahitajika maandalizi ya muda mrefu, juhudi na ushirikiano wa kidugu. “Asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi... Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia... Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine” (1Tim 3:6; 4:16; 5:22).
 
Wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua [[wanaume]] tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa [[Bikira Maria]], mtakatifu kuliko wote. “Petro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake... Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya... kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja” (Mdo 1:13-14,23,26). “Walimchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao” (Mdo 6:5-6).
 
Kutoa daraja kwa wanaume tu si kuwakosea haki wanawake, kwa kuwa hizo ni huduma zinazofaidisha wote. “Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye” (Lk 22:27). Mwenye daraja anahudumia Kanisa kwa kumwakilisha Yesu; hivyo anatakiwa kuwa mwanamume kama yeye mbele ya Bibiarusi wake. Kukubali mgawanyo wa majukumu maishani ni kusifu [[hekima]] ya Mungu aliyetuumba watu wa [[jinsia]] mbili tofauti ili kustawisha [[familia]], [[jamii]] na Kanisa. “Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana... Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor 11:11; 12:27).
 
Mwenye daraja anaweza kuwa na [[ndoa]]. “Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?” (1Kor 9:5). Paulo, akiwa [[mseja]], hakudai kila mmojawao aoe, ila asiwe ameoa mara mbili, bali “mume wa mke mmoja” (1Tim 3:2; Tit 1:6), kama alivyoagiza mjane aandikishwe akiwa tu “mke wa mume mmoja” (1Tim 5:9). Polepole mang’amuzi yakaelekeza Kanisa kubana nafasi hiyo kwa Maaskofu, na katika ma[[jimbo]] mengi kwa mapadri pia. [[Useja mtakatifu]] unawalinganisha zaidi na Yesu na kuwaachia [[uhuru]] wa moyo na wa muda kwa ajili ya huduma. “Wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee” (Math 19:12).
 
==Vyeo vingine visivyo sakramenti==