Tofauti kati ya marekesbisho "Isa"

35 bytes added ,  miaka 12 iliyopita
d
roboti Nyongeza: zh:伊斯兰教中的耶稣; cosmetic changes
d (roboti Nyongeza: zh:伊斯兰教中的耶稣; cosmetic changes)
Yeye ni miongoni mwa mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahimilivu wao mkubwa: Manabii [[Nuhu]] na [[Ibrahim]] na [[Musa]] na Isa na [[Muhammad]]. Tena ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili. "Masihi Isa bin Mariamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Neno lake tu alilompelekea Mariamu, na ni Roho iliyotoka kwake" (sura ya 4 aya 171). Wakristo wanamuita kwa kawaida [[Yesu Kristo]].
 
== Kuzaliwa kwake ==
 
Nabii Isa alizaliwa na bibi Maryam kimiujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimtuma malaika Jibrili kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa, alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwingine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mamake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba. Huu ni mfano mmoja katika mifano minne ya uumbaji aliyotuonyesha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu bila ya baba wala mama, na akamuumba Hawa bila ya mama, na akamuumba Isa bila ya baba, na akaumba wanadamu wote waliobakia kutokana na baba na mama.
 
 
== Ujumbe wake ==
 
Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahili kuabudiwa kwa haki, na ujumbe huu ndio ujumbe uleule uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu ili kuwaongoza, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kuzipa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Kadiri ya sura ya 3 aya ya 50 alisema ni "msadikishaji wa yale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na ili niwahalalishieni baadhi ya yale mliyoharimishiwa, na nimewajieni na Ishara kutoka kwa Mola wenu, kwa hiyo mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii". Alitabiri kuwa baada yake atakuja Mmoja ambaye atawafundisha wanadamu ukweli wote na kuwaongoza kwenye haki na kuwaeleza kila wanalolihitaji katika maisha yao. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ule wa Mtume Muhammad ambao ndio wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote.
 
== Kitabu cha Nabii Isa ==
 
Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya uongozi na sharia na hekima kwa wafuasi wao. Katika vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii mbalimbali ni Taurati kwa Nabii Musa, Zaburi kwa Nabii Daudi, Injili kwa Nabii Isa, na Qurani kwa Nabii Muhammad. Kitabu cha Nabii Isa kiliteremshiwa Wayahudi ambao ndio walengwa wake wa kwanza wa Nabii Isa, kama ilivyothibitishwa na Qurani wakati aliposema:
:''Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi!''
 
== Miujiza ya Nabii Isa ==
 
Nabii Isa alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbalimbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa ni kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuhu na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbalimbali. Baadhi ya miujiza ya Nabii Isa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ni kuumba ndege kutokana na udongo, kuponyesha vipofu wakaweza kuona, na kuwaondoshea ukoma wale wenye ukoma, na kuhuisha mtu aliyekufa, na kuwateremshia wafuasi wake chakula kutoka mbinguni ili iwe ni dalili kwao wote.
 
== Imani ya Kikristo kuhusu Isa ==
 
Muhammad alikuta Wakristo au Manasara wakiwa wamehitilifiana katika imani yao kuhusu Nabii Isa, kwani wote walimkiri kuwa Mwana wa Mungu, lakini kwa wengi hii ilikuwa na maana kuwa yeye ni Mungu aliyejifanya mtu, isipokuwa wachache walitafsiri tofauti. Makundi ya namna hiyo yalitengana baada ya Nabii Isa kuondoka ulimwenguni na kuwaachia wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada ya wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walitoa fikra na mawazo yao kuhusu Isa, hivyo baada ya muda waligawanyika makundi mbalimbali.
 
== Kurudi kwa Nabii Isa ==
 
Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake aliyoiacha baada ya kupaa kwenda kwa Mola wake, na haya yanaelezwa katika vitabu vya dini vya Kiislamu na vya Kikristo, lakini wanahitilifiana kuhusu namna na njia aliyoondokea ulimwenguni. Waislamu wanasema kuwa Isa alichukuliwa na Mola wake na kupandishwa kwake mbinguni baada ya Wayahudi kutaka kumuua, na kwa hivyo hawakuweza kumuua wala kumsulubu. Wakristo kwa upande mwingine, wanaamini kuwa aliwahi kusulubiwa na kuzikwa kisha akafufuka siku ya tatu. Muhimu hapa ni kujua kuwa atarudi tena duniani kukamilisha kazi aliyopewa na Mwenyezi Mungu.
 
[[CategoryJamii:Dini]]
[[CategoryJamii:Uislamu]]
[[CategoryJamii:Manabii katika Uislamu]]
 
[[ar:المسيح عيسى بن مريم]]
[[tr:İslam'da İsa]]
[[ur:عیسیٰ علیہ السلام]]
[[zh:伊斯兰教中的耶稣]]
44,086

edits