New England : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
nyongeza na masahihisho
No edit summary
Mstari 4:
 
==Historia==
Eneo hili lilikuwa chanzo cha ukoloni wa Uingereza katika [[Amerika ya Kaskazini]]. Mpelelezi mwingereza John Smith alitembelea nchi mnamo mwaka 1614 akatoa kitabu "A Description of New England" alipoeleza uwingi wa samaki, ubao na ardhi yenye rutba akisema nchi ilifaa kuunda "Uingereza Mpya" katika sehemu hizi. Maelezo yake yalianza kuvuta walowezi wachache walionunua ardhi kutoka kwa maindio wenyeji na kujenga makazi yao.

Tangu 1629 walowezi hao waliongezeka sana kutokana na uhamisho wa Wakristo waliowahi kujitenga katika kanisa rasmi la Uingereza na kuteseka huko. Walipewa nafasi ya kuhama Amerika walipoahidiwa uhuru wa kidini.

Walowezi walipanusha eneo lao ama kwa njia ya mapatano na wazalendo au kwa njia ya vita. Mara nyingi walowezi walianza kulima mashamba mapya nje ya sehemu za koloni ndogo za awali; kama walishambuliwa na wazalendo wasiokubali kulima kwao jeshi la miji ya koloni liliingia kati na kwa mdaasa wa silaha za Kiulaya kushinda makabila ya wenyeji. kwa njia hii maeneo ya walowezi yalipanuka polepole. Uwingi wa ardhi ya kulimia uliendelea kuvuta walowezi wapya na koloni hizi za Uingereza zilistawi kwa kuuza mazao kwenda Ulaya.
 
==Viungo vya Nje==