Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with 'thumb|right|300px|Mchoro wa mtaguso wa kwanza wa [[Konstantinopoli.]] '''Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli''' ndio wa pili katika orodha y...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:33, 16 Agosti 2009

Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ndio wa pili katika orodha ya mitaguso ya kiekumene ya Kanisa wakati wa mababu. Uliitishwa na kaisari Teodosius I ukafanyika Konstantinopoli mwaka 381.

Mchoro wa mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli.

Maaskofu 150 waliohudhuria walilaani aina mbalimbali za uzushi, hasa ule wa Masedoni wa Konstantinopoli aliyekanusha umungu wa Roho Mtakatifu, na kuthibitisha maamuzi ya mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso wa kwanza wa Nisea), uliofanyika mwaka 325.

Hivyo walikiri kwamba Roho Mtakatifu pia, kama vile Yesu Mwana wa Mungu, anachanga hali ileile ya Baba.

Pamoja na hayo, walikamilisha kanuni ya imani ya Nisea ambayo kwa sababu hiyo inaitwa sasa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli na ambayo inatumika sana hata leo katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika liturujia.

Viungo vya nje