Grafolojia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: sl:Grafologija
No edit summary
Mstari 1:
'''Grafolojia''' pia huitwa '''elimu ya mwandiko'''.
 
Tangu zamani sana, watu kadhaa wa [[China]], [[India]], [[Ugiriki]] na [[Italia]] walivutiwa na jinsi [[mwandiko]] wa kila mmoja ulivyo tofauti na ule wa wengine, wakaona unadokeza nafsi yake. Kuanzia [[karne XVII]] vilianza kutungwa vitabu kuhusu suala hilo, mpaka ikakubalika sayansi ya mwandiko (grafolojia) inayochunguza uhusiano kati ya mwandiko wa mtu na undani na nafsi yake (akili, maelekeo, vipawa, [[umbo]], [[maradhi]] n.k.). Msingi wake ni kwamba hatuandiki kwa [[mkono]] tu, kwa kuwa huo unaongozwa na [[ubongo]]. Mtu anapoacha kuiga [[herufi]] alizofundishwa kwa kuwa amezoea kuandika, anakuja kutokeza nafsi yake mwenyewe katika upekee wake. Tunaweza kusema mtu anapoandika bila ya kuzingatia usanifu wa herufi anajichora jinsi alivyo.
 
Wataalamu wa [[fani]] hiyo wanazingatia hasa kama mwandiko ni wa mviringomviringo au una [[pembe]] na [[ncha]], unakandamiza [[karatasi]] kwa nguvu au la, ni mkubwa au mdogo, ni mpana au mwembamba, unapendeza kwa ulinganifu wa herufi zake au la, unafanyika kwa kasi au polepole, unakwenda wima ingawa karatasi haina mstari au huenda ukapanda ama kushuka, unaelekea upande gani, una mapambo au la, n.k.
 
Kila sifa ya mwandiko ina sababu yake na hivyo kudokeza silika ya mtu upande wa akili, utashi n.k. Lakini baada ya kuzizingatia zote ni muhimu kuziona zote kwa pamoja ili kumtambua mtu mzima jinsi alivyo, na hatimaye kumsaidia maishani.
 
[[CategoryJamii:Elimu]]
[[Jamii:Mwandiko]]
[[Jamii:Saikolojia]]
 
[[ar:جرافولوجي]]