Benedikto wa Nursia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with ''''Benedikto wa Nursia''' (480-547) alikuwa mmonaki wa Italia aliyeandika kanuni ya utawa iliyoenea katika monasteri nyingi za Kanisa la Kilatini ...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 18:32, 10 Oktoba 2009

Benedikto wa Nursia (480-547) alikuwa mmonaki wa Italia aliyeandika kanuni ya utawa iliyoenea katika monasteri nyingi za Kanisa la Kilatini na hata nje yake. Wanaoifuata wanaitwa Wabenedikto.

Anaheshimiwa kama mtakatifu abati.

Wabenedikto wanaadhimisha sikukuu yake tarehe ya kufa, lakini kalenda ya Kanisa la Roma inaiadhimisha tarehe 11 Julai tangu Papa Paulo VI alipomtangaza msimamizi mkuu wa Ulaya tarehe 24 Oktoba 1964. Waorthodoksi wanamuadhimisha tarehe 14 Machi.

Maisha

Benedikto da Nursia, pacha wa Mtakatifu Skolastica, alizaliwa tarehe 12 Septemba 480, katika familia tajiri ya Roma. Baba yake, Eutropius Anicius, alikuwa kapteni mkuu wa Warumi katika eneo la Nursia, wakati mama yake alikuwa Claudia Abondantia Reguardati, malkia mdogo wa kijiji hicho.

Aliishi miaka ya utoto kijijini Nursia, akiathiriwa na wahamiaji kutoka Dola la Roma la mashariki ambao katika karne III walikimbia dhuluma wakashika maisha ya kiroho katika mapango waliyojichimbia mwambani kandokando ya kanisa dogo.

Alipofikia umri wa miaka 12 hivi mapacha walitumwa Roma kwa masomo, lakini alichukizwa na anasa za jiji hilo, alivyosimuliaPapa Gregori I katika kitabu cha pili cha Majadiliano. Hivyo akaacha masomo, nyumba na mali ili avae kanzu ya kimonaki akampendeze Mungu tu.

Alipofikia miaka 17 alitawa kwenye bonde la mto Aniene karibu na Eufide (leo Affile), halafu alielekea Subiaco, alipokutana na mmonaki wa monasteri ya jirani ambayo abati yake Adeodatus alimvika kitawa akamuonyesha pango kwenye mlima Taleo.

Huko aliishi miaka 3 kama mkaapweke hadi Pasaka ya mwaka 500. Halafu akakubali kuongoza wamonaki wengine karibu na Vicovaro, lakini, baada ya kunusurika kuuawa kwa sumu, akarudi Subiaco, alipobaki karibu miaka 30, akihubiri neno la Mungu na kupokea wanafunzi wengi zaidi na zaidi, hata akawa anaongoza monasteri 13, kila mojawapoi kiwa na wamonaki 12 na abati.

Karibu na mwaka 529 baada ya upinzani mkali wa padri jirani aliyejaribu kumuua na kupotosha wafuasi wake, aliamua kuhama akaelekea Cassino ambapo, juu ya mlima alianzisha monasteri ya Montecassino juu ya mabaki ya mahekalu ya Wapagani.

Kanuni

Huko Montecassino Benedikto alitunga kanuni yake mwaka 540 hivi. Akifaidika na zile zilizotangulia, hasa Regula Magistri iliyoandikwa na mmonaki asiyejulikana, lakini pia ya Basili Mkuu, Yohane Kasiano, Pakomi na Sesari, aliunganisha nidhamu na heshima kwa mtawa na vipawa vyake, ili kuunda shule ya utumishi wa Bwana ambapo kauli-mbiu ni ora et labora ("sali na kufanya kazi").

Hadi kifo chake aliishi Montecassino, akitembelewa na waamini na watu maarufu kama Totila mfalme wa Ostrogoti. Alifariki tarehe 21 Machi 547, siku arubani hivi baada ya Skolastica ambaye wakazikwa katika kaburi moja.