Mkataba wa Helgoland-Zanzibar : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Badiliko: en:Heligoland–Zanzibar Treaty; cosmetic changes
Mstari 3:
Mkataba yalihusu maeneo katika Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kusini-Magharibi na Afrika ya Magharibi (Togo) pamoja na kisiwa cha [[Helgoland]] mbele ya pwani la Ujerumani katika [[Bahari ya Kaskazini]].
 
== Shabaha ya Mkataba ==
Shabaha kuu ya mkataba ilikuwa kuondolewa kwa hatari za magongano kati ya Ujerumani na Uingereza. [[Leo von Caprivi]] alikuwa [[chansella]] mpya wa Ujerumani tangu Machi 1890 akimfuata [[Otto von Bismarck]]. Caprivi alitaka kujenga uhusiano mwema hasa na Uingereza.
 
Wakati huohuo uhusiano ule ulikuwa mashakani kidogo kutokana na matendo ya [[Karl Peters]] aliyejaribu kupanusha eneo la [[Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki]] hadi [[Uganda]] kinyume cha mapatano ya mwaka 1886 kati ya Ujerumani na Uingereza juu ya mipaka ya maeneo chini ya athira yao katika [[Afrika ya Mashariki]].
 
== Afrika ya Mashariki ==
Uingereza ilikubali koloni ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] ([[Tanganyika]], [[Rwanda]], [[Burundi]]. Waingereza waliahidi kumshawishi Sultani ya Zanzibar ili awaachie Wajerumani haki za Zanzibar Tanganyika bara.
Ujerumani ilifuta mipango yake katika [[Uganda]] na [[Zanzibar]] ambako Mjerumani [[Karl Peters]] aliwahi kusaini mapatano ya ushirikiano na [[Usultani wa Zanzibar|Sultani]] na [[Kabaka]].
 
Pia iliwaachia Waingereza Usultani ya [[Witu]] iliyokuwa tayari chini ya ulinzi wa Ujerumani tangu 1885 na madai yake kwenye pwani la Kenya katika eneo la [[funguvisiwa ya Lamu]] na pwani la [[Somalia]] hadi [[Kismayu]].
 
== Afrika ya Kusini-Magharibi ==
Pande zote mbili zilipatana kuhusu utawala wa Kijerumani katika eneo ambalo lilikuwa [[Namibia]] baadaye. Wajerumani walikubali kutovuka mstari wa [[mto Oranje]] upande wa kusini na kukubali utawala wa Waingerezea juu ya [[Botswana]]. Wajerumani walipewa pia njia ya kufikia [[Mto Zambezi]] katika kanda lililoitwa baadaye [[Kishoroba cha Caprivi]].
 
== Afrika ya Magharibi ==
Pande zote mbili zilipatana mipaka kati ya koloni zao za [[Togo ya Kijerumani]] na "Pwani la dhahabu la Kiingereza" ([[Ghana]]) halafu kati ya [[Kamerun]] na "eneo la Kiingereza linalopakana" ([[Nigeria]]).
 
== Ulaya ==
Uingereza iliachia Ujerumani kisiwa cha [[Helgoland]] katika [[Bahari ya Kaskazini]]. Kisiwa hiki kiliwahi kuchukuliwa na Uingereza wakati wa vita dhidi ya [[Napoleon]] mwaka 1807 ikawa koloni ya Kiingereza. Kisiwa kilidaiwa na Ujerumani kwa sababu kihistoria ni sehemu ya jimbo la [[Frisia ya Kaskazini]] lililokuwa sehemu ya Ujerumani baada ya kuhamishwa mara kadhaa kati ya Ujerumani na [[Denmark]].
 
 
[[CategoryJamii:Historia ya Afrika]]
[[CategoryJamii:Zanzibar]]
[[CategoryJamii:Ukoloni wa Ujerumani]]
[[CategoryJamii:Ukoloni wa Uingereza]]
 
[[de:Vertrag zwischen Deutschland und England über die Kolonien und Helgoland]]
[[en:Heligoland-ZanzibarHeligoland–Zanzibar Treaty]]
[[es:Tratado de Heligoland-Zanzíbar]]
[[fr:Traité Heligoland-Zanzibar]]