Western : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: sr:Вестерн
d roboti Nyongeza: ast:Western; cosmetic changes
Mstari 5:
Filamu za Western zilitengenezwa baadaye pia huko [[Ulaya]] hasa [[Spaghetti Western]] na mara nyingi zilicheza na aina za wahusika jinsi zilivyokuwa kawaida katika filamu za Marekani.
 
== Mazingira ya kihistoria ya filamu hizi ==
Katika nyakati zile Marekani ilitawala sehemu za mashariki za Amerika ya Kaskazini tu na kupanua polepole kuelekea magharibi hadi kufikia [[Pasifiki]] na baadaye pia kutawala maeneo ya katikati. Palikuwa na eneo la "mpakani" (''frontier'') ambako wakulima walowezi na wafugaji kutoka Marekani waliingia katika nchi ya wakazi asilia au [[Maindio]] na kuanzisha makazi yao huko. Mashamba na miji yale yalikuwa nje ya eneo la Marekani yenyewe. Kwa hiyo maisha yalikuwa kwa muda bila sheria wala serikali. Hata kama maeneo mapya yaliingizwa katika [[Maungano ya Madola ya Amerika]] taasisi za serikali zilikuwa mbali kwa muda na kazi ya kuratibu maisha ilibaki mkononi wa watu wenyewe katika eneo fulani.
 
[[ImagePicha:Buffalo Bill's Wild West Show.jpg|thumb|300px|Macowboy kazini]]
 
== Wahusika katika hadithi za Western ==
Hadithi zinazosimuliwa katika filamu za western mara nyingi huwa na watu wafuatao:
* '''Cowboy''' au mchunga ng'ombe - anayeonyeshwa mara nyingi kama mtu mwenye kazi ngumu asiye na elimu lakini ni hodari. Kwa kawaida ni mtu mwema.
* '''Sheriff''' au mpolisi - anayepigana na waovu; huishi na kulala ofisini mwake anapoangalia pia wafungwa. Kazi yake ni pamoja na kutetea wafungwa wale kama watu wa mji wanataka kuwanyonga mara moja. Kwa kawaida ana uwezo wa kutumia bunduki yake haraka sana. Huwa ni mtu mwema.
* '''Rancher''' au mwenye shamba la mifugo - yeye ni mwajiri wa macowboy. Ama ni mtajiri sana au yeye ni maskini anayeanza kujenga maisha yake na kupambana na matatizo ya kila aina. Mara nyingi ni mtu mwema lakini hutokea pia kama mbaya anayetaka kujitajirisha hata akimwua jirani
* '''Watu wa mjini''' - ama mwenye duka au mwenye kilabu. Anahofia waovu wanaopita mjini na kupora pesa zake. Kwa kawaida huwa mwoga asiye tayari kumsaidia sheriff.
Mstari 24:
*'''Mwovu mkuu na wenzake''' ni pilipili na sukari ya filamu za Western. Wanafika kutoka nje na kuleta kifo mpaka wameuawa wenyewe.
**Mara wanashambulia benki mara wanafuata mipango ya kulipiza kisasi kwa sababu sheriff wa mji aliwahi kumwua kaka wa mwovu mkuu miaka 23 iliyopita. Wengine wameajiriwa na rancher mbaya kumfukuza jirani wake mwema kwa sababu chemchemi ya pekee iko ndani ya eneo lake.
**Wakati mwingine mwovu huonyeshwa kuwa na tabia nzuri kwa sababu ameshakata shauri kuacha maovu lakini kwa bahati mbaya tangazo lenye picha yake linaloahidi kiasi cha pesa kwa yeyote anayemkamata au kumwua liko katika ofisi ya sheriff. Kwa hiyo sheriff anapaswa kumwinda. Kama sheriff angependelea kutomwona au kumsahau kuna mwovu wa aina nyingine ni headhunter au mwindaji wa waovu wanotafutwa anayetaka kichwa chake kwa sababu ya pesa.
[[ImagePicha:The searchers Ford Trailer screenshot (25).jpg|thumb|300px|Macowboy na Maindio (bado hai)]]
*'''Mmeksiko''' ni mtu mdogo asiyeongea Kiingereza sanifu ni mtu anayestahili kupigwa na kudharauliwa na macowboy. Kosa lake ni ya kwamba miaka kadhaa iliyopita alishindwa na Waamerika na kubaki kwenye nchi iliyovamiwa na Marekani. Katika mawestern za baadaye mara chache anapata nafasi ya kumwua mwovu pia.
 
*'''Indio''' au mwenyeji asilia wa Amerika ni hatari. Anaiba mifugo na kushambulia ovyo wazungu wazuri Wamarekani. Kama mkurugenzi wa filamu ana pesa ya kuajiri waigizaji wa kutosha maindio wengi sana hushambulia nyumba ya rancher au hata mji wote wakikaribia kushinda lakini kwa bahati nzuri '''cavallery''' (jeshi la farasi) hufika na kuwafukuza. Katika Western za baadaye inaweza kutokea ya kwamba sababu za Waindio zaelezwa kwa nini wanashambulia kwa mfano kwa sababu Wamarekani walitwaa ardhi yao au kuua watoto wao. Lakini hii si lazima kwa sababu marafiki wa filamu za Western hupenda kuona maajabu ya Western hawapendi kutafakari mno.
 
== Maajabu ya Western ==
Tabia ya ajabu ya watu katika filamu hizi ni wakifika mjini baada ya kusafiri njia ndefu kwa farasi kwenye jua kali huingia mara moja kilabuni. Hapa hawanywi maji au angalau bia lakini mara moja pombe kali ya whiskey wakiagiza chupa kimoja ([[lita]] 0.7).
 
Mstari 37:
 
{{DEFAULTSORT:Western}}
[[CategoryJamii:Filamu]]
[[CategoryJamii:Filamu za Marekani]]
[[CategoryJamii:Filamu za Western]]
 
{{Link FA|pt}}
 
[[ar:وسترن]]
[[ast:Western]]
[[bg:Уестърн]]
[[ca:Western]]