Dhambi ya asili : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 2:
 
==Dhambi ya Asili katika Biblia==
[[Image:Forbidden fruit.jpg|thumb|300px|[[Michelangelo]] alivyochora katika kuta za [[Cappella Sistina]] huko [[Vatikano]] [[dhambi]] ya [[Adamu na Eva]] na [[adhabu]] iliyofuata ya kufukuzwa bustanini.]]
 
[[Kitabu cha Mwanzo]] sura ya 3 inasimulia dhambi hiyo. Kwa njia ya [[hadithi]] hiyo tunaambiwa hali yetu mbaya haitokani na [[Mungu]], bali na uasi wetu na wa wazee wetu ([[Hek]] 2:23-24). Pia tunafundishwa kukataa toka mwanzo vishawishi vyetu tukiamini maagizo yote ya Mungu yametolewa kwa upendo mkuu.
 
[[Shetani]] ndiye aliyeanzisha [[kishawishi]]. [[Eva]] alipaswa asimsikilize. Kosa lake la kwanza ni kumjibu: hivyo shetani akamdanganya kwamba, eti Mungu ana [[kijicho]], hataki watu walingane naye, ndiyo sababu aliwakataza ([[Yoh]] 8:44). Tukianza kuzingatia kishawishi tunakubali shaka juu ya wema wa Mungu kwetu katika kutuelekeza. Kwa namna hiyo walianguka watu wa kwanza waliokuwa watakatifu; kwa urahisi zaidi tutaanguka sisi wenye tabia mbaya kutokana na dhambi hiyo na nyingine nyingi.
 
Hata baada ya dhambi Mungu anamtafuta mtu kwa upendo, ila huyo kwa aibu anamkimbia, au akijisikia analaumiwa na [[dhamiri]], basi anatafuta visingizio hata kumlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyesababisha. Kwa utakatifu wake Mungu hawezi kuvumilia maovu, na kwa haki yake anataka makosa yalipwe. Ndiyo sababu tunakuta matatizo maishani, kama vile uchungu wa uzazi, kuhusiana kwa mabavu, kupata riziki kwa shida, na hasa kufa: hayo yote ni matokeo ya dhambi.
 
Pamoja na hayo Mungu hapendi mtu yeyote apotee ([[2Pet]] 3:9), hivyo toka mwanzo aliahidi kwamba mzawa wa Eva atamponda kichwa shetani ([[Mwa]] 3:15). Ndiyo habari njema ya awali kuhusu wokovu ujao.
 
==Maendeleo ya dhambi==
 
Baada ya dhambi ya asili watu walianza kuzaa. Mwa 4:1-16 inatuchorea picha ya [[Kaini]] na [[Abeli]] kama wazaliwa wa kwanza waliotofautiana kiadili ([[1Yoh]] 3:11-12). Toka mwanzo mwovu na mwadilifu waliishi pamoja, wa kwanza akimdhulumu wa pili hata kumuua bila ya kujali udugu. Ikisikitishwa kufikiria mzaliwa wa kwanza kuwa muuaji wa mdogo wake, inafurahisha kwamba wa kwanza kufa alikuwa mwema, kielelezo cha [[Yesu]] aliyeuawa bila ya kosa ([[Eb]] 12:24).
 
Toka mwanzo hao walimuabudu Mungu kwa njia ya [[dini]], [[ibada]] na [[sadaka]] mbalimbali. Hata hivyo Mungu akakubali zile tu zilizotolewa kwa ukarimu (Eb 11:4). Tangu hapo [[Biblia]] inatuonyesha jinsi alivyopendelea wadogo kuliko wakubwa.
Line 28 ⟶ 29:
[[Category:Biblia]]
[[Category:Ukristo]]
[[Jamii:Maadili]]
 
[[ar:الخطيئة الأصلية]]