Mfalme : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''Mfalme''' ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa ...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 18:56, 2 Februari 2007

Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.

Utawala wa kifalme ilikuwa hali ya kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu.

Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia".

Hakuna utaratibu sanifu mtawala gani anastahili kuitwa "mfalme". Kwa kawaida anasimamia eneo au nchi ya kujitegemea lakini wengine huweka pia mashariti kuhusu ukubwa wa eneo lake.

Kwa maeneo fulani kuna vipindi katika historia ambako si rahisi kutofautisha kati ya wafalme na watawala wadogo wengine.

Tazama pia: Kaisari, Mtemi