FORD-People : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 9:
 
==Kuundwa kwa Ford-P kutokana na farakano Matiba-Shikuku==
Kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 1997 faragano lilitokea katika chama cha [[FORD-Asili]] kati ya mwenyekiti [[Kenneth Matiba]] na [[Martin Shikuku]] aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama. [[Shikuku]] aliyekuwa na wafuasi wengi aliendelea kushikilia hatamu za ofisi ya chama. Nyumba ya ofisi ilikuwa mali ya Matiba aliyetimuliwa ofisi ya chama chake. Lakini Shikuku alienda akishika hati ya kusajiliwa kwa chama.
 
Upande wa kundi la Matiba, mwanasiasa [[Kimani wa Nyoike]] alikuwa Katibu Mkuu. Bila mawasiliano na [[Matiba]][[wa Nyoike]] aliandikisha chama kipya kwa jina la [[Ford-People]] kwa sababu aliogopa kubaki bila chama iwapo [[Shikuku]] angefaulu kutetea haki ya kumiliki jina la Ford-Asili. [[Matiba]] alikata tamaa kuhusu hali ya siasa na akajiondoa katika shughuli zote za kisiasa nchini [[Kenya]]. Hivyo [[wa Nyoike]] alibaki na chama alichokuwa akiandaa kwa upande wa [[Matiba]] lakini bila kiongozi huyu.<ref>[http://www.nationaudio.com/elections/politicalparties/Party1.htm Will Nyoike sell Nyachae? - taarifa ya "Nation" 13-05-2002 ilisomwa tar. 5.01-2008]</ref>