The Sixth Sense : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Badiliko: pt:O Sexto Sentido
Mstari 28:
Mwanzoni mwa filamu, Dk. Malcolm Crowe ([[Bruce Willis]]) mwanasaikolojia mashuhuri wa watoto, amerejea nyumbani kwake usiku mmoja akiwa na mkewe, Anna Crowe ([[Olivia Williams]]), wakiwa wanatokea katika sherehe za ugawaji wa tuzo za madaktari ambamo naye alipewa tuzo hizo akiwa kama daktari bora wa watoto.
 
Wawili hao wakagundua ya kwamba hawapo peke yao - Vincent Grey ([[Donnie Wahlberg]]), mgonjwa wa zamani wa Crowe, akionekana katika njia ya mlango wa kuelekea bafuni kwao akiwa na silaha huku akisema, "Sitaki kuwa naogopa tena." Grey anamlaumu Crowe kwa kushindwa kumtibia yeye, na Crowe akamtambua Vincent kama mgonjwa wake wa zamani ambaye alimtibia mara moja wakati wa utoto wake alivyokuwa akisumbuliwa na [[hallucinationndoto]]. Grey akamtandika Crowe risaidi ya tumbo, halafu baadaye akajitandika mwenyewe risasi ya kichwa. Kipande hicho kimeishia Crowe na mkewe akiwa yupo pembeni yake.
 
Sehemu ya pili inaonyesha Crowe anafanya kazi na kijana mwingine, mwenye umri wa miaka tisa - Cole Sear ([[Haley Joel Osment]]), mwenye hali sawa na ile ya Vincent. Crowe ikambidi ajitolee muhanga kwa mgonjwa huyu, ingawa bado alikuwa na shaka juu ya uwezo wake ni hasa baada ya kushindwa kumtibia Vincent. Baada mda mfupi, akaanza kuonekana dhahiri kuwa hashuhuriki na mkewe, ambaye baadaye mahusiano yao yakaja kupagalanyika.