Shaka Zulu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: hu:Saka Zulu
d roboti Nyongeza: fiu-vro:Shaka; cosmetic changes
Mstari 1:
[[ImagePicha:KingShaka.jpeg|thumb|right|Picha ya Shaka Zulu mnamo mwaka 1824]]
'''Shaka''' (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: '''Shaka Zulu''', Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 [[BK]]) alikuwa kiongozi wa [[Zulu|Wazulu]] aliyebadilisha ukoo mdogo wa [[Nguni|Kinguni]] kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya [[Afrika Kusini]] hasa [[Natal]] ya leo.
 
Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake. Sifa hizi, jinsi ilivyo mara nyingi na viongozi wanaotegemea nguvu ya kijeshi, zimeenda pamoja na vita na uharibufu mwingi. Miaka ya Shaka ilianzisha kipindi cha [[mfecane]] yaani "uharibifu" kinachokumbukwa na mataifa mengi ya Afrika Kusini.
 
== Maisha yake ==
 
=== Kijana ===
Shaka alikuwa mtoto wa chifu [[Senzangakhona ka Jama]] na [[Nandi]] binti wa chifu wa [[Langeni]]. Jina lake ni kutokana na neno la kizulu "iShaka" linalomtaja mdudu ambaye katika imani ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga hedhi ya wakinamama. Jina hili ni dalili la kuzaliwa nje ya utaratibu. Hivyo miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba anayejulikana rasmi akisikia kudharauliwa na watu wengine. Utoto huu ulisababisha hasira ndani yake akalipiza kisasi baadaye.
 
Kama kijana Shaka alikaa kwa kabila kubwa zaidi ya [[Mthethwa]] alikoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule ukoo wa Wazulu walikubali Wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthethwa alikuwa [[Dingiswayo]] aliyeanzisha utaratibu mpya wa [[impi]] yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi mbalimbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka sita katika vita za Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi alioboresha baadaye.
 
=== Kurudi kwa Wazulu ===
Baada ya kifo cha babake Shaka alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza kisasi maadui wa utoto wake akiwaua kwa njia mbalimbali.
 
Shaka aliendelea kukubali ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo hadi huyu aliuawa vitani na kabila la [[Ndwandwe]] mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na koo au makabila madogo jirani. Mbinu yake ilikuwa kuwashambulia waliompinga au kuwa hatari kwake; wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na wanajeshi wa kiadui wasiouawa lakini waliokubali kumfuata baada ya kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa Wazulu uliendelea kukua.
 
=== Kupanusha utawala na [[mfecane]] ===
Baada ya kifo cha Dingiswayo mw. 1817 Shaka alishambulia kabila kubwa la Ndwandwe akawashinda kwenye mapigano ya kilima cha Gqokli kwa sababu ya mbinu zake za kijeshi ingawa idadi ya watu wake ilikuwa nusu tu ya adui.
 
Katika miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundi vya jirani na kuwaingiza katika utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita wakikubali uongozi wake na kuingiza vijana wao katika impi au vikosi vya kijeshi vya Shaka. Alituma viongozi au majenerali zake pamoja na impi pande mbalimbali hadi [[Msumbiji]] au pia Zimbabwe. Vikundi kama Ndebele huko [[Zimbabwe]] au hata [[Wangoni]] katika [[Tanzania]] ni matokeo ya matembezi ya impi za kizulu zilizoenda mbali na kupoteza mawasiliano na nyumbani.
 
Vita hizi zilisababisha makabila mengine kukimbia na kuhamahama wakishambulia majirani zao hivyo kupanusha eneo la vita katika nchi mbali na Wazulu wenyewe. Kipindi hiki kinakumbukwa kwa majina kama "mfecane" ([[Kizulu]]) au "difaqane" ([[Kisotho]]) kuwa miaka 30 ya vita na kifo.
 
Katika mawazo ya wataalamu Shaka aliandaa upanuzi wa [[Makaburu]] kwa uharibifu wa vita zake. Makaburu walipoanza kuenea ndani ya Afrika Kusini walikuta maeneo mazuri bila watu lakini maghofu ya kuonyesha watu waliwahi kuishi hapa. Pamoja na hayo makabila mengine kama [[Wasotho]], [[Waswazi]], [[Wandebele]] au [[Wagaza]] walioshambuliwa walijifunza mbinu za kijeshi wakifaulu kujitetea na kuanzisha mataifa makubwa yakiunganisha wenyewe koo na makabila madogo zaidi.
 
=== Kifo ===
Utawala wa Shaka ulikuwa na tabia za kinyama zilizosababisha chuki nyingi dhidi yake. Baada ya kifo cha mamake Nandi alikuwa na hasira kiasi cha kuua watu 7000 kati ya wanajeshi wake kwa kosa la kutoonyesha huzuni ya kutosha na kuamuru kipindi cha kufunga miezi mitatu. Aliamuru mashamba yasilimwe kwa mwaka mmoja na kila mwanamke aliyeonekana kuwa na mimba katika kipindi hiki aliuawa pamoja na mumewe. Wataalamu wengine huona ya kwamba wakati ule Shaka alionekana kuwa na kichaa. Maadui walifanya mipango dhidi yake mwishowe aliuawa na ndugu zake. Mwaka 1828 impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikuli ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangana walimwua na kutupa maiti shimoni.
 
Mstari 31:
 
 
== Mafanikio ya kijeshi ya Shaka ==
Shaka aliboresha utaratibu alioukuta katika utumishi wa Dingiswayo. Wataalamu hutofautiana ni kiasi gani ya kwamba Shaka alianzisha mbinu kadhaa au kiasi gani ndiye Shaka aliyeunganisha mbinu mbalimbali zilizowahi kujulikana lakini yeye alifuata utaratibu kuzitumia kushinda viongozi wote wengine. Kati ya mbinu alizotumia ni zifuatazo:
 
=== Silaha mpya ===
Utamaduni wa Wanguni ulikuwa mikuki ya assegai na kila mtu alibeba tatu. Shaka aliona silaha za kutupwa ni hasara. Aliongea mwenyewe na wahunzi akawapa wanajeshi silaha katikati ya mkuki na upanga - "Iklwa". Haikufaa kutupwa bali kushikwa hivyo kuwalazimisha watu wake kushambulia na kuwa karibu na adui. Aliwapatia pia vigao vizito vya ngozi ya ngòmbe.
 
=== Kutembea bila viatu ===
Alilazimisha watu wake kuacha vyandalua na viatu na kutembea pekupeku. Hii iliongeza kasi ya impi zake na uwezo wao wa kushambulia haraka. Inasemekana ya kwamba Shaka aliua wote waliolalamika walipoamriwa kuacha viatu vyao.
 
=== Kujenga nidhamu ===
Shaka alijenga nidhamu ya watu wake kwa kuwa na utaratibu wa mamlaka kati yake mwenyewe na vikosi vidogo zaidi. Sehemu nyingine ilikuwa adhabu kali: askari asiyeweza kuonyesha damu kwenye silaha yake aliweza kuuawa baada ya kurudi vitani. Impi ambazo zilipata sifa machoni pa Shaka ziliruhusiwa kuoa baada ya ushindi.
 
=== Kuwa na vikosi vya kusaidia mizigo ===
Shaka alitumia wavulana wadogo kuanzia umri wa miaka sita waliongozana na impi wakibeba mizigo au kuwafuata wanajeshi kwa ngombe kama chakula. Hata hii iliharakisha mwendo wa impi zake.
 
=== Impi za hirima ===
Hirima au vikundi vya kujumuisha watu wa umri moja ni tabia ya utamaduni kwa Wabantu wengi. Shaka alipoanzisha impi zake -badala ya kushambulia na watu wake wote mara moja jinsi ilivyokuwa kawaida awali- alitumia vikundi vilivyokuwepo tayari kiutamaduni kama msingi wa impi zake.
 
=== Muundo wa Kichwa cha Mbogo ===
Shaka alitumia mpangilio wa impi zake vitani kwa umbo la "Kichwa cha Mbogo":
1. vikosi viwili upande wa kushoto na kulia vilikuwa kama "pembe za mbogo"
2. kikosi kikubwa cha katikati kilikuwa kama "uso" au "kifua"
3. vikosi vya ziada au vya wazee vilikuwa "viuno" vilivyotumika ama kuongeza uzito wa mashambulio panapohitajika au kuimarisha utetezi pale ambako adui alisogea mbele.
 
[[CategoryJamii:Afrika Kusini]]
 
[[CategoryJamii:HistoriaViongozi yawa Afrika]]
[[Category:Afrika Kusini]]
[[CategoryJamii:ViongoziHistoria waya Afrika]]
[[Category:Historia ya Afrika]]
 
[[af:Shaka]]
Line 76 ⟶ 75:
[[eu:Shaka Zulu]]
[[fi:Shaka Zulu]]
[[fiu-vro:Shaka]]
[[fr:Chaka Zulu]]
[[ga:Shaka Zulu]]