Vifaa vya Deni (Soko la Hisa la Nairobi) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with 'Kifaa cha deni ni mkopo. Mwombaji hupa ahadi ya kulipa interest fulani kila robo au nusu mwaka kwanzia tarehe Fulani baada ya kupata mkopo huo na pia uahidi kulipa mkopo aliyopew...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:51, 14 Januari 2010

Kifaa cha deni ni mkopo. Mwombaji hupa ahadi ya kulipa interest fulani kila robo au nusu mwaka kwanzia tarehe Fulani baada ya kupata mkopo huo na pia uahidi kulipa mkopo aliyopewa. Hivyo basi, faida kutoka kwa kifaa cha deni hutokana na interest. Kwa sasa hivi, vifaa kadha za deni zina interest rate ya 14%, 12%, 01%, 8% kutegemea na aina ya kifaa hicho na siku iliosajiliwa. Katika Soko la Hisa la Nairobi waweza kununua na kuuza vifaa vya deni.

Ni nani anayeweza Kuomba fedha

Nchini Kenya, makampuni na serikali ndiyo yanaweza kuomba fedha kupitia vifaa vya deni katika soko la hisa. Katika masoko mengine ya hisa, hospitali, vyuo vikuu, mashule na organizations zingine pia zaweza omba fedha kupitia njia hii ikiwa wanaaminiwa na umma.

Kununua Kifaa Cha Deni

Katika Soko la Hisa la Nairobi bei ya chini zaidi ya kununua kifaa cha deni ni KShs. 100,000. Unaponunua kifaa cha deni cha kampuni Fulani, basi wewe huwa umekopesha kampuni hiyo fedha iliyosambamba ba bei ya vifaa vya deni ulivyonunua.

Ni nani anayeweza kununua

Mtu yeyote wa kibinafsi, Kampuni ya Uwekezaji, Kanisa, Shule, Chuo Kikuu, Kampuni ya Bima na institution mengine mengi.

Kuuza Kifaa Cha Deni

Wakati wa mahitaji ya kighafla, mwekezaji anaweza kuuza vifaa vya deni alivyonunua katika soko kwa urahisi kwani faida ya kifaa cha deni huongezeka kila siku hivyo basi huwa na bei mpya kila siku. Hivyo basi, mwekezaji anaweza kuuza vifaa vyake vya deni siku yoyote kabla ya siku yake ya kukomaa bila kutozwa faini yoyote. Hata hivyo, panapokuwa na wauzaji wengi katika soko, bei ya vifaa vya deni hushuku na kasha kupanda wanapopungua.

Angalia pia

Viungo vya nje