Machafuko darfur : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
(Hakuna tofauti)

Pitio la 07:47, 21 Januari 2010

Machafuko ya Darfur yalianza katika eneo la Darfur, Sudan, mnamo Februari mwaka wa 2003 wakati ambapo Jeshi la Ukombozi la Sudan na Harakati ya Haki na Usawa zilichukua silaha na kuanza kushutumu serikali kwa kuwadhulumu Waafrika huku ikiwapendelea Waarabu. Kuna makadirio mbalimbali ya idadi ya watu waliowawa. Upande mmoja ambao unajumuisha jeshi la Sudan na Janjaweed, kundi la wanamigambo lenye wapiganaji kutoka makabila ya Abbala ambayo ni mchanganyiko wa Waarabu na Waafrika wa kanda ya kaskazini katika eneo la Rizeigat la Sudan.

Mama na mtoto wake mgonjwa katika kambi ya walifurushwa makwao ya Abu Shouk katika eneo la Kaskazini la Darfur.


Makabila haya haswa ni wachungaji mifugo wa kuhamahama ambao huchunga wanyama kama vile ngamia. Upande mwingine ulikuwa wa makundi ya kiasi, hasa Jeshi la Ukombozi la Sudan na Harakati ya Haki na Usawa, ambayo yalipata wapiganaji kutoka maeneo ya makabila ambayo si ya Kiarabu na ambayo ni ya Kiislamu kama vile Fur, Zaghawa, na Masalit. Serikali ya Sudan, ingawa imekana hadharani kuwa haiwasaidii wanamigambo wa Janjaweed, inashutumiwa kwa kuwasaidia wqapiganaji kifedha, na kwa kuhusika katika mashambulizi ya pamoja yanayolenga raia.

Serikali ya Sudan imelaumiwa kwa kuharibu ushahidi, kama vile kufunika makaburi ambapo watu wengi wamezikwa. Pia serikali hiyo imewakamata na kuwanyanyasa wanahabari, hivyo kufanya ripoti za habari kutoka eneo la Darfur kuwa chache.

Ingawa serikali ya Marekani imeufafanua mgogoro katika eneo hilo kama mauaji ya kimbari, Umoja wa Mataifa haujatambua mgogoro huo hivyo. Mnamo tarehe 31 Januari, mwaka wa 2005, Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ya kurasa 176 ikisema kuwa ingawa kulikuwa na mauaji kwa wingi na ubakaji wa raia wa eneo la Darfur, haingeweza kuyatambua mateso hayo kama "mauaji ya kimbari" kwa sababu "nia ya kufanya mauaji ya kimbari haikuwepo".

Wanaharakati wengi, hata hivyo, wanatambua mgogoro katika eneo la Darfur kama mauaji ya kimbari, kama vile mashirika ya Save Darfur Coalition, Aegis Trust na Genocide Intervention Network. Mashirika haya yanaashiria matamshi ya Katibu Mkuu wa zamani wa Marekani Colin Powell, yaliyotambua mgogoro kama mauaji ya kimbari. Mashirika mengine ya kiharakati, kama vile Amnesty International, ingawa yanaomba hatua ya kimataifa ichukuliwe, wanakataa kutumia maneno mauaji ya kimbari.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Machafuko darfur kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.