Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Mfumo wa Mmeng'enyo wa Chakula''' ni mfumo katika [[mwili wa binadamu]] na [[mamalia]] wengine unaohusika na umeng'enyaji wa [[chakula]] mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. Ili chakula kiweze kutumika mwilini, ni lazima kivunjwevunjwe kiwe katika hali rahisi ya kuweza kusharabiwa. Kazi hiyo hufanywa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wa mwanadamu hufanana na ule wa [[sungura]], [[panya]] naau [[pimbi]]. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng’enyaji huo ni [[kinywa]], [[umio]], [[mfuko wa tumbo]], [[ini]], [[mfuko wa nyongoonyongo]], [[utumbo mwembamba]], [[kongosho]], [[utumbo mpana]] na [[puru]].
Mmeng’enyo wa chakula ni kitendo cha kubadili chakula kutoka hali tata isiyoweza kusharabiwa kuwa katika hali rahisi inayoweza kusharabiwa na mwili. Chakula kinaposafiri katika njia yake hufanyiwa [[mabadiliko ya kiumbo]] na [[mabadiliko ya kikemikali]]. Kila sehemu ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ina kazi maalum.
Chakula cha mnyama au binadamu huweza kuwa cha [[kabohaidreti]]/[[wanga]], [[protini]], [[fati]] au mchanganyiko wa vyakula hivyo. Myeyuko wa makundi hayo ya vyakula hutokea katika sehemu mbalimbali za [[njia ya chakula]] kwa njia za kemikali.
 
==Mmeng’enyo Kinywani==
 
Kinywa ni sehemu ya kwanza kupokea chakula. Chakula kinapokuwa mdomoni huvunjwavunjwa na kusagwa na [[meno]]. Mate husaidia kukilainisha. [[Ulimi]] husaidia kugeuzageuza chakula hicho na kukiviringisha kuwa tonge.
 
===Meno===
 
[[Meno]] huvunjavunja chakula na kuwa vipande vidogovidogo wakati wa kutafuna na kusaga. Hivyo chakula huwa katika vipande vipande ambavyo huongeza eneo zaidi kwa shughuli za umeng’enyaji zinazofanywa na [[vimeng’enya]] vinavyopatikana katika [[njia ya chakula]]. Vilevile meno husaidia kufanya chakula kuwa rahisi kumezwa.
 
===Mate===
 
[[Mate]] ni mchanganyiko wa [[maji]], uteute na kimeng’enya kinachofahamika kama ''salivary amylase'' au [[ptyalin]]. Kazi za mate katika umeng’enyaji ni kama ifuatavyo:
* Maji yaliyo katika mate hutumika katika kuyeyusha chakula.
* Uteute wake hulainisha chakula hivyo chakula huwa rahisi kumezwa.
* Kimeng’enyo chake ([[ptyalin]]) hubadili [[wanga]]/[[kabohaidreti]] kuwa sukari rahisi (''maltose'').
 
===Ulimi===
 
[[Ulimi]] huzungusha zungusha [[chakula]] na huwa kama tonge. Kwa msaada wa [[ulimi]], tonge hilo husukumwa kuelekea kwenye [[umio]] (kiingereza huitwa ''oesophagus''). Chakula kinapoingia katika [[umio]], huelekea kwenye [[mfuko wa tumbo]]. Vyakula rojorojo hupita kwa haraka zaidi kuliko vyakula vizito.
 
==Mfuko wa tumbo==
 
Chakula huhifadhiwa katika mfumo[[mfuko wa tumbo]]. Mfuko huo una uwezo wa kupanuka wakati unapopokea chakula na kusinyaa unapokuwa hauna chakula. Chakula huwa katika tumbo mwa muda wa saa tatu hadi nne. Muda huu hutegemea aina ya chakula. Chakula cha [[kabohaidreti]], kwa mfano [[uji wa mahindi]], huwa tumboni kwa muda usiozidi saa moja. Chakula cha [[protini]] kwa mfano [[nyama]], huweza kuwa tumboni kwa muda wa saa moja au mbili.
Katika mfuko wa tumbo, kuta za tumbo zina tezi (''gastric glands'') zitoazo misusumo ya gastriki (''gastric juice'') ambayo huwa na aside[[asidi ya haidrokloriki]], uteute na kimeng’enya. Vimeng’enya vinavyotolewa tumboni ni ''[[pepsinogen]]'' na ''[[prorennin]]''.
 
===Asidi ya Haidrokloriki===
 
Asidi ya haidrokloriki husaidia kufanya mambo yafuatayo tumboni:
* Husaidia kuweka mazingira ya asidi ili vimeng’enya vya tumbo viweze kufanya kazi. Vimeng’enya vya tumboni hufanya umeng’enyaji kwa ufanisi katika hali ya uasidi.
* Huvunja sukari tata (complex sugar) kuwa sukari rahisi.
* Huuwa [[bakteria]] walio katika chakula.
* Huanzisha ufanyaji kazi wa vimeng’enyo vingine katika [[tumbo]]. [[Pepsinogen]] na [[prorennin]] hubadilishwa kutoka katika hali ya awali na kuwa [[pepsin]] na [[rennin]] kwa mpangilio uliotajwa; hali ambazo ndizo hasa hufanya umeng’enyaji.
 
===Pepsin===
 
[[Pepsin]] humeng’enya chakula cha [[protini]] na kuwa [[peptides]]. Pepsin hutolewa katika namna ya [[pepsinogen]]. Namna hii haiwezi kufanya mmeng’enyo mpaka itakapokutana na asideasidi; hivyo kuzuia kumeng’enya [[seli]] zinazoitoa katika tezi za tumbo.
 
===Rennin===
 
[[Rennin]] hugandisha [[protini]] iliyo katika [[maziwa]] ili kimeng’enya cha pepsin kiweze kuivunja protini kwenda katika [[peptides]]. Kimeng’enya hiki pia hutolewa katika namna ya [[prorennin]], ambacho huhitaji pia asidi ile kiweze kufanya kazi yake. Kimeng’enya hiki hupakitana sana katika matumbo ya mamalia wachanga walio katika [[kipindi cha kunyonya]].
 
===Uteute===
 
Uteute wa tumbo hulinda kuta za tumbo ili zisikwanguliwe na asidi ya haidrokloriki na pepsin. Bila uteute huu tumbo linaweza kujimeng’enya linyewe. Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya uteute huu, asidi ya haidrokloriki na ugonjwa wa [[vidonda vya tumbo]] (''ulcers'').
 
===Kazi za tumbo===
 
Kwa ufupi kazi za tumbo ni kama ifuatavyo:
* Hutumika kama sehemu ya kutunzia chakula kwa muda mfupi kabla ya kuendelea umeng’enywaji katika sehemu zingine za mfumo wa chakula.
* Umeng’enywaji wa chakula cha protini huanzia katika tumbo.
* Kwa kutumia misuli yake, tumbo husaidia katika kuchanganya chakula na misusumo ya tumbo, hivyo kuboresha zoezi la umeng’enyaji tumboni.
* Usharabiwaji wa [[maji]], alkoholi na baadhi ya [[vitamin]] hutokea katika tumbo. Mfuko wa tumbo una misuli ambayo husinyaa na kutanuka mara nyingi, hivyo kwa muda wote chakula kinapokuwa kwenye mfuko huo huchanganywachanganywa. Kitendo hicho pamoja na athari za misusumo iliyopo kwenye mfuko wa tumbo husababisha kufanyika kwa tuitumbo (kiingereza huitwa ''chyme'').
 
==Utumbo mwembamba==
 
Kutoka kwenye mfuko wa tumbo, chakula huelekea kwenye [[utumbo mwembamba]]. Utumbo mwembamba ni mrefu zaidi kuliko [[ogani]] nyingine yoyote ya njia ya chakula. Chakula huwa ndani ya utumbo mwembamba kwa muda mrefu zaidi kuliko sehemu nyingine za nia ya chakula. Katika utumbo mwembamba chakula hukutana na misusumo yenye vimeng’enya ambavyo hutoka kwenye kongosho na utumbo mwembamba. Vimeng’enya hivyo husaidia kuyeyusha chakula.
Utumbo mwembamba umegawanyika katika sehemu mbili, [[duodenum]] na [[ileum]].
 
===Duodenum===
Mstari 64:
====Ini====
 
[[Ini]] ni ogani kubwa kuliko ogani zingine katika mwili wa binadamu. Ini huweka akiba ya chakula kama vile aina za [[wanga]] iitwayo [[glaikojeni]], [[vitamin]] na [[chumvi za madini]]. Ini pia hutengeneza nyongo ambayo husaidia katika mmeng’enyo wa fati. Nyongo hufanya kazi zifuatazo:
* Huvunja vunja [[fati]] (''lipids'') na kuwa vipande vidogovidogo ambavyo huongeza nafasi kwa vimeng’enya vingine viweze kufanya kazi zao.
* Huweka hali ya alkali ambayo ni mazingira mazuri kwa vimeng’enya vya utumbo mwembamba kufanya kazi.
* Kuondoa asidi iliyo katika tuitumbo iliyoipata wakati chakula kilipo tumboni.
 
====Kongosho====
 
Misusumo inayotengenezwa na [[kongosho]] hufikia chakula kwa kutumia mfereji unaounganisha duodenum na kongosho. Misusumo ya kongosho huwa na vimeng’enya vifuatavyo
* ''Pancreatic amylase'': hii huvunjavunja [[wanga]]/[[kabohaidreti]] iliyobaki kwenda katika ''maltose''.
* ''Pancreatic Lipase'': humeng’enya vipande vidogovidogo vya fati na kuwa asidi za fati na glaiserini (''glycerol'').
* ''Trypsin'': Huvunja protini iliyobakia na kuwa [[peptides]]. Trypsin hutolewa katika namna ya ''trypsinogen''.
* ''Sodium Hydrogen Carbonate'' (NaHCO<sub>3</sub>): Huweka hali ya alkali ambayo ni mazingira mazuri kwa vimeng’enya vya utumbo mwembamba kufanya kazi.
 
===Ileum===
 
Hii ni sehemu ya pili ya utumbo mwembamba ambayo ni ndefu sana na imekunjakunja sana. Sehemu imejikunja ili iweze kutosha sehemu ya tumbo ambayo ingekuwa ndogo kama ungenyooka (inafikia karibia mita saba). [[Ileum]] hutoa misusumo yenye vimeng’enya vifuatavyo:
* ''Erepsin'' (peptidase): Humeng’enya peptides na kuwa [[asidi za amino]].
* ''Maltase'': Huvunja ''maltose'' na kuwa ''glucose''.
* ''Lipase'': humeng’enya vipande vidogovidogo vya fati na kuwa asidi za fati na [[glaiserini]] (''glycerol'').
* ''Sucrase'': Huvunja ''sucrose'' na kuwa glucose.
 
Mchakato wa umeng’enyaji humalizikia kalizikia katika ileum. Ileum kwa ujumla ina kazi kuu mbili:
Mchakato wa umeng’enyaji humalizikia kalizikia katika ileum. Ileum kwa ujumla ina kazi kuu mbili: Umeng’enyaji wa [[kabohaidreti]], [[protini]] na [[fati]]. Pia usharabiwaji wa chakula ambacho ni matokea ya umeng’enyaji kwenda katika [[mkondo wa damu]].
Umeng’enyaji wa kabohaidreti, protini na fati.
Usharabiwaji wa chakula ambacho ni matokea ya umeng’enyaji kwenda katika mkondo wa damu.
Kusharabiwa kwa chakula
Chakula kinapofikia hatua hizo huwa kiko tayari kusharabiwa na vinywelea vilivyo katika utumbo mwembamba viitwavyo [[vilasi]]. Vilasi hizo huchukua [[asidi za amino]], sukari rahisi (glucose) na chumvi na kupeleka katika mishipa ya vena hadi kwenye [[ini]]. Katika ini sukari rahisi hubadilishwa kuwa [[glaikojeni]] na kuhifadhiwa. Asidi za amino za ziada hugeuzwa kuwa glaikojeni na yurea(kemikali fulani ambayo baadaye huwa mkojo). Kutoka kwenye ini chakula kinachohitajiwa na mwili husafirishwa na damu hadi kwenye moyo. Damu hiyo husambaza chakula hicho katika mwili mzima kwa matumizi mbalimbali.
Sehemu kubwa ya chakula humeng’enywa na kusharabiwa katika [[utumbo mwembamba]]. Chakula kilichobaki huelekea kwenye [[utumbo mpana]].
 
==Utumbo mpana==
Mstari 98:
 
==Viungo vya Nje==
 
[http://www.vivo.colostate.edu/hbooks/pathphys/digestion/ Mfumo wa Umeng'enyaji]
[http://science.nationalgeographic.com/science/health-and-human-body/human-body/digestive-system-article.html National Geographic - Mfumo wa Umeng'enyaji]
[http://en.wikipedia.org/wiki/Digestion Umeng'enyaji katika Wikipedia ya Kiingereza]
 
==Marejeo==
Line 103 ⟶ 107:
# Mwaniki, J. M. (2008) Fundamentals of Biology Second Edition, Delah Educational Publishers, Dar es Salaam
# Taasisi ya Ukuzaji Mitaala, Sayansi, Kitabu cha Nne, Eastern Africa Publications Limited
# [http://digestive.niddk.nih.gov/ddiseases/pubs/yrdd/index.htm Namna Mfumo wa Umeng'enyaji Unavyofanya kazi]
 
[[Jamii:Bailogia]]