Karani tamba : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with '{{Uainishaji | rangi = mweupe | jina = Karani tamba | picha = Sagittarius serpentarius -Kalahari-8-4c.jpg | upana_wa_picha = 250px | maelezo_ya_picha = Karani tamba | himaya ...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:50, 29 Januari 2010

Karani tamba
Karani tamba
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Accipitriformes
Familia: (R. Grandori & L. Grandori, 1935)
Jenasi: Sagittarius
(J. F. Miller, 1779)


Karani tamba (Sagittarius serpentarius) ni ndege mkubwa wa ardhini ambaye huwinda wanyama wengine. Yeye hupatikana katika maeneo mengi Barani Afrika, mara nyingi katika maeneo tambarare na katika maeneo ya nyika ya Afrika.


Ingawa yeye anajumuishwa katika oda ya Accipitriformes, ambayo ni ya ndege wengi wawindaji wanaoonekana mchana kama vile mwewe, shavikale, tai na kipondya, yeye anapewa familia yake ya kipekee iitwayo, Sagittariidae.

Yeye huonekana katika nembo ya nchi za Sudan na Afrika Kusini.

Sifa

 
katika Bustani ya Wanyama ya San Diego, Marekani
Karani tamba anatembea alikofungiwa katika bustani ya wanyama ya Ueno Zoo

Karani tamba anafahamika wazi kutokana na mwili wake unaofanana wa tai, na miguu yake inayofanana ya korongo, inayomfanya aonekana mrefu zaidi hata kufikia urefu wa mita 1.3 (futi 4). Ndege huyu mwenye urefu wa sentimita 140 (futi 4.5) ana kichwa kinachofanana cha tai na mdomo uliojipinda kwenda chini, lakini ana mabawa ya mviringo.[1]


Uzani wake wa wastani ni kilo 3.3 (paundi 7.3) na upana wa mabawa ni mita 2 (futi 6.6).[2] Kwa sababu ya miguu yake mirefu na mkia wake mrefu, yeye ni mrefu kuliko ndege yeyote mwingine wa kuwinda wakati wa mchana.[3]

Kwa umbali au anapopaa angani, yeye hufanana korongo bali si ndege wa kuwinda. Mkia una manyoya mawili marefu yanayoonekana kuwa marefu kuliko miguu yake anapopaa, na pia mkusanyiko wa manyoya yanayotengeneza umbo kama la nundu.[1] Manyoya ya kupaa ya karani tamba na mapaja yake ni meusi, huku manyoya mengine yakiwa rangi ya kijivu na mengine yakiwa meupe.[4] Ndege wa kiume na kike wanafanana kwani spishi huyu ana tofauti chache sana za kijinsia, ingawa ndege wa kiume ana manyoya marefu zaidi ya kichwani na manyoya marefu ya mkia. Ndege waliokomaa wana uso mwekundu usiokuwa na manyoya, wakitofautishwa na makinda wenye ngozi ya manjano katika nyuso zao.[1]


External links


  1. 1.0 1.1 1.2 Eagles, Hawks, and Falcons of the World, Volume 2 - Brown, L. & Amadon, D. New York: McGraw-Hill Book Company (1968)
  2. Raptors of the World - Ferguson-Lees, J.; Houghton Mifflin, New York. 978-0618127627 (2001)
  3. Ferguson-Lees & Christie, Raptors of the World. Houghton Mifflin Company (2001), ISBN 978-0618127627
  4. Birds of Africa: South of the Sahara - Sinclair, I. & Ryan, P., Princeton and Oxford: Princeton University Press (2003)