Morgunblaðið : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with '{{Infobox gazo | jina = Morgunblaðið | jina la gazeti = Morgunblaðið | picha = Picha:Morgunbladid frontpage1.jpg | aina = Gazeti la kila siku<small>'''Tangu mwaka ...'
 
No edit summary
Mstari 18:
}}
==Historia==
'''''Morgunblaðið''''' (Swahili: ''Gazeti la Asubuhi'') ni gazeti linalochapishwa katika nchi ya [[Iceland]],lilianzishwa na Vilhjálmur Finsen & Olaf Björnsson. Toleo la kwanza lilikuwa na kurasa nane tu lilichapishwa tarehe 2 Novemba, 1913. Miaka sita baadaye, katika mwaka wa 1919,shirika la Árvakur likanunua kampuni hiyo. Jarida hili lilikuwa na uhusiano wa karibu na chama cha Independence, hasa wakati wa [[Vita Baridi]]. Wahariri wake na wanaripoti wake wa bunge waliketi katika mikutano ya bunge mpaka mwaka wa 1983,wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Árvakur alikuwa ,pia, Mwenyekiti wa chama cha Independence,Geir Hallgrímsson. Kulikuwa na uamuzi kuwa uhusiano huo haungesaidia chama au gazeti hilo kwa njia yoyote. Ingawa uhusiano na chama cha Independence sio wa moja kwa moja kama ule wa miongo iliyopita, jarida hili hukosolewa kwa kuegemea msimamo wa chama hicho hasa katika misimu ya uchaguzi. Jarida hili huwa na maadili ya kihafidhina sawa na yale ya chama cha Independence na limeonyesha msimamo huru katika masuala kadhaa muhimu kama mjadala kuhusu usambazaji wa haki za uvuvi. Hivi majuzi, gazeti hili limechukua hatua ya kuajiri wanahabari waliochukua msimamo wa kuegemea sera za ''kushoto'' na gazeti hili limeendeleza sera za kutetea haki za wanawake katika kurasa zake.
 
Tangu chapisho lake la hapo awali, ''Morgunblaðið'' halikuchapishwa Jumatatu lakini baada ya muda lilijiundia jina kama gazeti bora. Lilikuwa gazeti bora kabisa nchini Iceland siku nyingi huku likiongoza kabisa katika mwanzo wa miaka ya 1970 na likashinda magazeti mengine yote kwa mbali katika wakati huo.Miongo mitatu iliyofuata, gazeti hili liliongoza bila ushindani wowote mkali. Katika wakati huu wa mafanikio, ''Morgunblaðið'' lilianzisha sehemu maalum kuhusu fedha, uvuvi, vyakula na kadhalika. Baada ya usambazaji wa bure (magazeti yakiwasilishwa hadi nyumbani mwa watu), gazeti la ''Fréttablaðið'' lilileta ushindani kwa kuanzisha toleo la Jumatatu. ''Morgunblaðið'' likaitikia changamoto na tangu mwaka wa 2003 likachapishwa kila siku ya wiki, likiwa na kurasa mbalimbali kati ya kurasa 60 na kurasa 120. Matangazo huchukua asilimia 30 - asilimia 40 ya nafasi ya makala. Usambazaji wa nakala wa kila siku ni kati ya 50,000 na 55,000, nyingi za hizi zikiwa zimeagizwa na watu. Usambazaji hulenga zaidi eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, hasa katika jiji kuu la [[Reykjavik]].