Macbeth : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with '250px|thumb|Picha ya tamthilia ya Macbeth. '''''Macbeth'' ''' ni tamthilia ya William Shakespeare inayohusu mauaji y...'
 
No edit summary
Mstari 1:
[[File:Thomas Keene in Macbeth 1884 Wikipedia crop.png|250px|right|thumb|Picha ya tamthilia ya Macbeth.]]
'''''Macbeth'' ''' ni tamthilia ya [[William Shakespeare]] inayohusu mauaji ya mfalme na athari yake. Ni [[tamthiliya fupi kabisa ya]] Shakespeare inayoaminika kuandikwa katika miaka kati ya 1603 na 1607.
 
Mstari 32:
==Kuhusu tamthilia hii==
[[File:Macbeth3.jpg|thumb|Macbeth pindi anapokumbana na wachawi]]
 
 
Tamthilia hii inaanza pindi wachawi watatu wanapokutana kujadiliana siku ambayo wataonana na Macbeth. Kuna radi na umeme. Baadaye, jeshi la Macbeth limeshinda vita dhidi ya jeshi la Norway. Macbeth, ambaye ni mkuu wa jeshi, anasifiwa kwa kazi yake.
 
Baadaye, Macbeth na Banquo wanakutana na wachawi watatu wanaomwambia Macbeth kuwa atakuwa kiongozi wa "Glamis" na wa "Cawdor" halafu baadaye atakuwa Mfalme. Baada ya muda kidogo tu, Ross, ambaye ni mtumwa wa Mfalme, anakuja kwa Macbeth na kumpa habari kuwa ametuzwa kwa kuwa Kiongozi wa "Cawdor". Maneno waliyosema wachawi yalianza kuwa ni ya ukweli. Papo hapo, Macbeth anafanya tamaa na kuwa na hamu ya kuwa Mfalme.
 
Kisha, anamwandikia mkewe barua kumwelezea kuhusu taarifa ya wachawi. Lady Macbeth anatunga njama ya kumuua Mfalme Duncan ili mumewe aupate ufalme. Ingawa Macbeth anaogopa kumuua mfalme, Lady Macbeth anamhimiza kwa kuchokoza ujanadume wake. Macbeth anakubali njama hii.
 
Usiku wa ziara ya mfalme katika nyumba ya Macbeth, Macbeth unamuua Duncan. Kulingana na mpango wake, anawasingizia watumishi wa Duncan waliolala kwa kuwaekea visu vilivyotapakaa damu. Mapema asubuhi iliyofuata, Lennox, ambaye ni diwani, na [[Macduff,]] ambaye ni kiongozi wa [[Fife,]] wanawasili. <ref> Angalia [[upande Knocking katika lango katika Macbeth.|''upande Knocking katika lango katika Macbeth.'' ]]</ref> Askari anawafungulia mlango na kisha Macduff anapatana na maiti ya Duncan huko ndani ya nyumba. Kwa hasira za unafiki, Macbeth anawaua walinzi kabla ya wao kujitetea. Macduff anashuku vitendo vya Macbeth, lakini hasemi kitu. Watoto wa Duncan wanakimbia nje ya nchi kwa hofu ya maisha yao. Macbeth anakuwa Mfalme wa Scotland.
 
Macbeth anawatuma watu wawili kuwaua Banquo na Fleance. Watu hawa wanamuua Banquo, lakini Fleance alitoroka. Baada ya muda, Macbeth hana raha kwa vitendo alivyovifanya. Macbeth anamshuku Macduff, hivyo basi anamuua mkewe Macduff na watoto wake.
 
Lady Macbeth anababaishwa na vitendo vya kikatili yeye na mumewe walivyofanya.. Yeye anaanza kubabaika mpaka akiwa usingizini, akiongea akisema mambo aliyoyafanya ilhali akiwa amelala.