Chungwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: sco:Oranger
No edit summary
Mstari 130:
[[zh-min-nan:Liú-teng]]
[[zh-yue:橙]]
 
 
'''Chungwa'''
 
Kutoka Wikipedia, ensaiklopidia huru
 
[[http://en.wikipedia.org/wiki/File:OrangeBloss_wb.jpg]]
machungwa na maua yake juu ya mchungwa.
 
==Utangulizi==
Chungwa, na hasa chungwa tamu, ni jamii ya matunda ya citrus, na huaminika kuwa yalikuzwa miongoni mwa enzi za pomelo na tangerine. Mti wake mdogo utoao maua hufikia urefu takribani mita kumi na majani yake yasiyokauka muda wote.
Machungwa asili yake ni huko kusini mwa Asia. Tunda lifahamikalo kisayansi kama Citrus sinesis huitwa chungwa tamu ili kutofautisha na Citrus aurantium, chungwa chungu.
 
 
==Tunda==
[[http://en.wikipedia.org/wiki/File:Orange_and_cross_section.jpg]] chungwa zima na kipande chake
 
matunda yote jamii ya jenasi ya citrus, huzaliana na familia yao hujumuisha machungwa, ndimu na limao. Matunda ya jamii hii huonwa kama ni ya ain aya beri sababu ya kuwa na mbegu nyingi, kuwa laini na nyama nyingi huku yakikua kutoka kwenye ovary moja.
 
 
==Kiwango cha asidi==
Kama ilivyo kwa jamii ya matunda ya citrus, machungwa nayo huwa na hali ya aside, yenye kiwango cha pH karibu na 2.5 -3, kulingana na umri wake, ukubwa na aina ya chungwa. Japo si kama ilivyo kwa limao, bado machungwa huwa na kiwango cha asidi cha kutosha, sawa kabisa na hata siki ya nyumbani.
 
 
==Uzalishaji==
[[http://en.wikipedia.org/wiki/File:2005orange.PNG]]
kiwango cha uzalishaji wa machungwa duniani.
 
Machungwa kwa kawaida hulimwa kwaajili ya biashara na hulimwa maeneo mengi duniani. Wazalishaji wa machungwa wanaoongoza duniani ni Brazili, Marekani na Meksiko. Machungwa huathirika kwa haraka sana na ukungu hivyo huhitaji matunzo mazuri pindi joto dogo sana linapotegemewa.
 
 
==Ulimaji==
[[http://en.wikipedia.org/wiki/File:Citrus_sinensis_JPG01.jpg]]
mti wa mchungwa.
 
Michungwa huweza kukuzwa maeneo yenye joto na hata yale yenye baridi. Kama ilivyo kwa matudna mengine ya citrus, ili kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika joto la 15.5°C - 29°C. Miti ya machungwa iliooteshwa kutokana na mbegu zilizonunuliwa madukani inaweza kuwa tofauti kabisa na ile miti ya asili iliyozalidha mbegu hizo. Hii hutokana na mabadiliko ya kizazi yanayotokana na kuchanganywa mbegu kisayansi kwa muda mrefu. Ili kupata mmea wa mchungwa kama tunda ulilolininunua, huna budi kuitunza mbegu hiyo kwenye unyevunyevu kisha tu baada ya kuzitua kwenye tunda na kuziotesha katika hali ya unyevu; na pindi mmea uchipuapo hapo ukapandwe kwenye udongo kusudiwa.
 
 
 
==Sharubati na bidhaa nyingine.==
[[http://en.wikipedia.org/wiki/File:Oranges_and_orange_juice.jpg]] machungwa na sharubati yake.
 
Machungwa yanakuzwa katika hali mbalimbali za joto duniani kote, na ladha yake hubadilika kuanzia hali ya utamu mpaka uchungu kabisa. Tunda kwa kawaida humenywa na kuliwa au huminywa na sharubati yake kunywewa. Limezungukwa na ganda lenye ladha chungu lakini huweza kukamuliwa na kuondolewa maji yake na kutumika kwa chakula cha mifugo. Pia hutumika kuongeza ladha ya vyakula vingine na hata maganda yake hufaa kwa kazi hii. Sehemu nyeupe ya ndani, kati ya nyama na ganda la nje nayo huwa na vitamini sawa kabisa na nyama ya ndani.
 
Sharubati ya machungwa ndiyo bidhaa kuu kuliko zote ya machungwa. Huweza kuzalishwa kwa matumizi ya nyumbani lakini hasa hufanywa kwa minajili ya biashara. Sharubati ya kugandishwa ya machungwa hutengenezwa kutokana na majimaji ya machungwa pia.
Mafuta ya machungwa ni bidhaa ndogo inayotengenezwa kwa kukamua maganda ya machungwa. Hutumika kwa kuongeza ladha ya chakula na zaidi kwenye utengenezaji wa manukato.
Maua ya machungwa nayo hupendwa kwa harufu yake nzuri na hutumika mara nyingi nyakati za harusi na huhusishwa na bahati njema.
Majani ya michungwa yanaweza kutumika kutengenezea chai. Maga