Karani tamba : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 30:
Karani tamba anafahamika wazi kutokana na mwili wake unaofanana wa tai, na miguu yake inayofanana ya korongo, inayomfanya aonekana mrefu zaidi hata kufikia urefu wa mita 1.3 (futi 4). Ndege huyu mwenye urefu wa sentimita 140 (futi 4.5) ana kichwa kinachofanana cha tai na mdomo uliojipinda kwenda chini, lakini ana mabawa ya mviringo.
 
Uzani wake wa wastani ni kilo 3.3 (paundi 7.3) na upana wa mabawa ni mita 2 (futi 6.6).''Raptors of the World'' - Ferguson-Lees, J.; Houghton Mifflin, New York. 978-0618127627 (2001)
 
Kwa umbali au anapopaa angani, yeye hufanana korongo bali si ndege wa kuwinda. Mkia una manyoya mawili marefu yanayoonekana kuwa marefu kuliko miguu yake anapopaa, na pia ana mkusanyiko wa manyoya yanayotengeneza umbo kama la nundu. Manyoya ya kupaa ya karani tamba na mapaja yake ni meusi, huku manyoya mengine yakiwa rangi ya kijivu na mengine yakiwa meupe.