Antibiotiki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: af, an, ar, bg, bn, bs, ca, cs, da, de, el, eo, es, et, fa, fi, fo, fr, gl, he, hr, hu, id, io, is, it, ja, kk, kn, ko, la, lt, mk, ml, mr, ms, nl, nn, no, oc, pl, ps, pt, qu, ro, ru, sh, simple, sk, sl, sr, sv, ta, th, tl, tr, uk, u
Mstari 1:
'''Antibaotiki''' (Kiingereza antibiotics, mara nyingine ''Kiua Vijasumu'') ni kemikali ambazo hutumika kuua au kuzuia ukuaji wa vijidudu vinavyosababisha magonjwa. Mwanzo neno ''antibaotiki'' lilitumika kuelezea kemikali zinazotengenezwa na [[bakteria]] au kalibu, ambazo ni sumu kwa viumbe wengine. Kwa sasa neno linatumika kujumuisha [[kampaundi za oganiki]] (kemikali za kaboni zinazopatikana katika viumbe hai) zinazotengenezwa na zile zinazopatikana kwa kuchanganya asilia na zile za bandia. Antibaotiki nyingi huwa ni sumu kwa [[bakteria]]; hatahivyo kwa kuwa neno limekuwa likituma pia kuelezea madawa ambayo hutumika pia kuzuia [[magonjwa]] kama [[malaria]], na yale yanayosabibishwa na [[virusi]] au [[protozoa]]. Antibaotiki zote zina tabia ya kuwa na uchaguzi inapotumika kama sumu. Zinakuwa hatari sana kwa viumbe vinavyoingia ndani ya kiumbe kingine kuliko vile zinavyokuwa ndani ya mnyama au binadamu ambaye hutumia kama tiba. [[Penicillin]] ni miongoni mwa antibaotiki zinazofahamika sana na imekuwa ikitumika kupambana na magonjwa mengi ya kuambukiza kama vile [[kaswende]], [[kisonono]] na [[pepopunda]]. Antibaotiki nyingine, ''[[streptomycin]]'' imekuwa inatumika kupambana na [[kifua kikuu]].
 
[[Picha:Penicillin.jpg|thumb|300px|right|Madawa ya antibaotiki]]
 
== Historia ==
 
Mwanzoni mwa muongo wa kwanza wa karne ya ishirini, mwanasayansi wa kijerumani [[Paul Ehrlich]] alianza majaribio na kampaundi za oganiki ambazo zingeweza kupambana na vijidudu vya magonjwa ya kuambukiza bila kumuumiza/kuathiri mwili wa kiumbe chenye ugonjwa. Majaribio yale yalipelekea katika mwaka [[1909]] kutengenezwa kwa ''[[salvarsan]]'', dawa iliyokuwa na [[arsenic]], ambao ilikuwa na tabia chaguzi juu ya ''[[spirochetes]]'', bakteria wanaosababisha [[kaswende]]. ''Salvarsan'' iliendelea kuwa matibabu pekee kwa [[kaswende]] mpaka ilipokuja [[penicillin]] katika miaka ya [[1940]]. Mnamo miaka ya [[1920]], Sir [[Alexander Fleming]] ambaye baadaye aligundua penicillin, aliona kitu kinachoitwa ''lysozyme'' katika misusumo mingi ya mwili kama vile [[machozi]] na [[jasho]], na katika mimea na wanyama fulani. Lysozyme ilikuwa na tabia zinazofanana na antibaotiki nyingi, lakini haikuwa na manufaa kimatibabu.
Mstari 10:
Tangu antibaotiki zilipokuwa zinatumika kwa matumizi ya kawaida katika miaka 1950 zimeleta mabadiliko makubwa. Magonjwa mengi ambayo mwanzoni yalikuwa yanaongoza katika kusababisha vifo kama vile [[kifua kikuu]], [[kichomi]] na ''[[septicemia]]'' yalianza kudhibitiwa. Shughuli za upasuaji pia ziliboreshwa kwa sababu shughuli ingeweza kufanyika kwa muda mrefu bila uwezekano wa maambukizi.
 
== Aina za Antibaotiki ==
 
Kuna antibaotiki nyingi sana kwa matumizi mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya antibaotiki maarufu na baadhi ya matumizi yake kiafya.
 
=== Penicillin ===
[[Picha:Penicillin_core.svg|thumb|300px|left|Penicillin ni antibaotiki ya kwanza ya asili kugunduliwa na Alexander Fleming]]
 
[[Penicillin]]s ni madawa yanayozuia ukuaji wa vijidudu (kiingereza bactericidal), ambayo hasa huzuia utengenezaji wa ukuta wa seli. Penicillin inafahamika sana kwa kuzuia utengenezaji wa ''polymer'' za ''peptidoglycan'' katika kuta za seli ya bakteria na huwa na ufanisi wakati kijidudu kinapotengeneza ukuta wa seli mpya (yaani wakati kinakua). Kuna aina nne za penicillins: ''[[penicillin-G]]'' za spektra nyembamba, ''[[ampicillin]]'' na aina zake, ''[[penicillinase-resistant]]'', penicillins kinzani kwa ''penicillianase'' (vimeng’enyo vinavyotolewa na bakteria fulani ili kuondo uwezo wa penicillin kutibu, na kupelekea kuwa sugu kwa antibaotiki hiyo), na penicillin za spektra iliyopanuka ambazo ni mahususi kupambana na ''pseudomonas''.
 
Penicillin-G zinatumika kutibu magonjwa kama vile [[kaswende]], [[kisonono]], [[homa ya uti wa mgongo]], [[kimeta]] na [[buba]]. Nyingine inayohusiana naye, [[Penicillin V]] inaweza kufanya kazi sawa lakini siyo madhubuti. ''[[Ampicillin]]'' na ''[[amoxicillin]]'' zina uwezo kama ule wa penicillin-G, lakini zina spectra pana zaidi inayohusisha bakteria wa gram hasi (gram-negative bacteria).
Mstari 23:
Madhara yanayotokana utumiaji, ingawa ni nadra kutokea, ni pamoja na mijibizo ya mzio (''allergic reactions'')-hasa, mabaka katika ngozi, homa na mshituko wa ghafla kutokana na kutumia dawa kwa mara ya pili (''anaphylactic shock'') ambao unaweza kusababisha kifo.
 
=== Cephalospin ===
 
Kama penicillins, [[cephalosporins]] zina muundo sawa (''B-lactam ring'') ambao unaweza kuvuruga utengenezwaji wa ukuta wa seli ya bakteria, hivyo zinyewe pia ni ''bactericidal''. Cephalosporins hutoa matokea mazuri zaidi ya penicillin dhidi ya ''[[bacilli]]'' wa gram hasi (gram-negative bacilli) na matokea sawa dhidi ya ''cocci'' wa gram chanya (gram-positive cocci). Cephalosporins inaweza kutumika kutibu aina mbalimbali za [[homa ya uti wa mgongo]]. Mara chache sana kumekuwa na matokea hasi pale cephalosporin zinapotumika kama harara za ngozi na mishituko y[a ghafla baada ya kutumia dawa kwa mara nyingine (''anaphylactic shock'').
 
=== Aminoglycosides ===
 
''Streptomycin'' ni ''[[aminoglycosides]]'' ya siku nyingi sana. Aminoglycosides zinazuia utengenezaji wa [[protini]] ya [[bakteria]] katika bakteria wengi wa gram hasi (gram-negative bacteria) na baadhi ya bakteria wa gram chanya (gram-positive bacteria). Kuna wakati mwingine hutumika pamoja na [[penicillin]]. Aminoglycosides nyingi huwa ni sumu kali kuliko antibaotiki zingine.
Mstari 33:
Madhara ambayo yanatokana na utumiaji wa aminoglycosides kwa muda mrefu ni kuharibika kwa eneo linalohusika na msawazo katika [[sikio]], ukiziwi na madhara ya [[figo]].
 
=== Tetracyclines ===
 
[[Tetracyclines]] huzuia utengenezaji wa [[protini]] za [[bakteria]]. Zenyewe ni antibaotiki za spektra iliyopanuka madhubuti kupambana na aina mbalimbali za ''streptococci'', ''bacilli'' za gram hasi (''gram-negative bacilli''), ''rickettsia'' (bakteria wanaosababisha [[homa ya matumbo]]-typhoid), na ''spirochetes'' (bakteria wanaosababisha [[kisonono]]). Hutumika kutibu magonjwa katika [[mfumo wa mkojo]] na [[koo]]. Kutokana na uwezo wao wa kuathiri [[bakteria]], wakati mwingine [[tetracyclines]] zinaweza kuvuruga uwiano wa bakteria ambao hutumika na mfumo wa kinga ya mwili, kwa mfano hupelekea maambukizi ya pili katika [[njia ya chakula]] (''gastrointestinal track'') na katika [[uke]]. Matumizi ya tetracycline yamekuwa ya kikomo kwa sababu kuna aina nyingi za bakteria ambazo huwa pinzani kwa dawa hizi.
 
=== Macrolides ===
 
[[Macrolides]] huzuia utengenezaji wa [[protini]] za bakteria kwa kujiunga na ''ribosomes'' za bakteria. ''Erythromycin'', miongoni mwa macrolides, hutoa matokea mazuri dhidi ya ''cocci'' za gram change (''gram-positive cocci'') na mara kadhaa imetumika kama mbadala wa [[penicillin]] dhidi ya maambukizi ya ''streptococci'' na ''pneumococci''. Matumizi mengine ya macrolides ni pamoja na kuwa tiba ya ''diphtheria'' na ''bacteremia''.
Mstari 43:
Athari zake zinaweza kuwa [[kizunguzungu]], kutapika, na kuharisha; na mara chache kutokusikia vizuri kwa muda fulani.
 
=== Sulfanomides ===
 
[[Sulfanomides]] ni antibaotiki za kutengeneza (siyo asilia kama ilivyo, kwa mfano penicillin) za spektra iliyopanuka madhubuti dhidi ya bakteria wengi wa gram chanya na hasi (gram-positive bacteria na gram-negative bacteria). Hatahivyo, kwa sababu bakteria wa gram hasi (gram-negative bacteria) wengi wamejenga ukinzani juu ya sulfonamides, kwa sasa antibaotiki hizi zimekuwa zikitumika katika kazi maalum kama kutibu maambukizi ya mfereji wa mkojo (''urinary-track infection'') dhidi ya aina za ''meningococci''.
Mstari 49:
Athari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ni kuingilia ufanyaji kazi wa [[Mfumo wa Mmeng'enyo wa Chakula|njia ya chakula]] (''gastrointestinal tract'').
 
== Utengenezaji ==
 
Utengenezaji wa antibaotiki huchukua muda mrefu na ni wa gharama sana. Kwanza, kiumbe kinachotengeneza antibaotiki inabidi kifahamike na antibaotiki hujaribiwa wa dhidi ya spishi mbalimbali za bakteria. Kisha kiumbe lazima kikuzwe ili kiweze kutoa antibaotiki kwa kiwango cha kutosha ili uchunguzi zaidi wa kikemikali uweze kufanyika kwa antibaotiki na kujaribu kuonyesha utofauti wake na zingine. Utaratibu huu ni tata kwa sababu kuna maelfu ya kampoundi ambazo hufanya kazi kama antibaotiki ambazo tayari zimeshagunduliwa, na bado zimekuwa zikirudiwa kugunduliwa tena. Baada ya antibaotiki kugunduliwa kufaa kwa ajili ya matumizi ya kutibu maambukizi katika wanyama, utengenezaji wa kiwango kikubwa huanza kufanyika.
Mstari 55:
Utengenezaji wa antibaotiki kwa ajili ya biashara huhitaji njia bora zaidi ili kupunguza gharama. Uchunguzi mkubwa huwa unahitajika ili kuongeza matokea kwa kuchagua aina fulani ya viumbe au kwa kubadili namna ya kuwakuza viumbe hao. Antibaotiki ilipatikana kwa njia za asili za uvundikaji inaweza kubadilishwa kikemikali ili kutengeneza antibaotiki zingine. Baada ya usafishaji, athari za antibaotiki kwenye ufanyaji kazi wa kawaida wa tishu na ogani za kiumbe kitakachoitumia (''pharmacology'') hujaribiwa kwenye idadi kubwa ya spishi za viumbe. Pia uwezekano wa kugeuka sumu (''toxicology'') katika viumbe hivi hujaribiwa. Zaidi namna ya utumiaji ambao utaleta matokeo mazuri lazima itafutwe. Zinaweza kutumiwa kwa mdomo. Hii inaweza kuwa kwa kuyeyusha au kumeza ambapo huja kusharabiwa kwenda kwenye [[mkondo wa damu]] kupitia [[utumbo]]. Pia zinaweza kutumia kwa njia nyingine zaidi ya mdomo kama kwa kuchoma dawa kwenye misuli au mishipa ya damu pale ambapo usharabiwaji wa haraka unahitajika.
 
Katika nchi ya [[Marekani]], mara tu hatua hizi zinapokamilika, mtengenezaji hutuma maombi kwenye utawala kupitia mamlaka ya chakula na madawa (Food and Drug Administration, FDA). Yakipitishwa, antibaotiki huweza kujaribiwa kwa sumu, ustahimilivu, usharabiwaji na utokaji mwilini. Kama majaribio haya kwenye idadi ndogo ya watu yatafanikiwa, dawa huwekwa kwa matumizi ya kundi kubwa la watu, mara nyingi huwa kama mamia ya watu. Hatimaye dawa hutumika kwa matumizi ya kawaida katika kliniki.
 
Taratibu zote hizi, kuanzia pale antibaotiki inapogunduliwa kwenye maabara mpaka inapoanza kutumika kwa majaribio kliniki mara nyingi huchukua muda mrefu-zaidi ya miaka kadhaa.
 
== Tahadhari na Vikomo ==
 
Matumizi ya antibaotiki yana vikomo kwa sababu [[bakteria]] wamekuwa wakibadili namna ya kujilinda dhidi ya antibaotiki fulani. Miongoni mwa njia kuu wanayotumia ni kuzimisha ufanyaji kazi antibaotiki. Hii ni njia ambao inatumiwa dhidi ya ''[[penicillin]]'' na ''[[chloramphenicol]]'' na nyinginezo. Aina nyingine ya kujilinda ni kubadilika (''mutation'') kwa vimeng’enyo vya bakteria vinavyoathiriwa na dawa kwa namna ambayo antibaotiki haziwezi kuzuia tena ukuaji (antibaotiki nyingi zina tabia chaguzi juu ya kipi cha kudhuru). Hii ndiyo namna pekee ambayo [[bakteria]] hutumia kujingika dhidi ya madawa yanoyozuia utengenezaji wa [[protini]] za bakteria kama vile ''[[tetracyclines]]''.
Mstari 67:
Vivyo hivyo, ''[[plasmodia]]'', kijidudu kinachosababisha [[malaria]], kimejenga ukinzani dhidi ya antibaotiki mbalimbali, wakati huo huo, [[mbu]] ambao wanabeba ''[[plasmodia]]'' katika miili yao, wamekuwa pinzani dhidi ya dawa za kuua wadudu ambazo zilikuwa zinatumika kuwaua. Matokeo yake ingawa malaria iliwahi kuonyesha dalili ya kupotea, sasa imeenea sana [[Afrika]], [[Mashariki ya Kati]], [[Asia Kusini]] na sehemu za [[Amerika ya Kilatini]]. Zaidi ya yote ugunduzi wa antibaotiki mpya sasa umekuwa siyo aghalabu kama ilivyokuwa zamani.
 
== Angalia Pia ==
 
* [[kifua kikuu|Kifua Kikuu]]
Mstari 75:
* [[Alexander Fleming]]
 
== Viungo vya Nje ==
 
* [http://familydoctor.org/online/famdocen/home/common/infections/protect/680.html Antibaotiki - Vitu inavyoweza na isivyoweza]
Mstari 82:
* [http://www.biotech.ntnu.no/molgen/research/antibiotics.html Utengenezaji wa Antibaotiki]
 
== Marejeo ==
 
# [http://users.rcn.com/jkimball.ma.ultranet/BiologyPages/A/Antibiotics.html Antibaotiki]
Mstari 88:
# Levy, Stuart B. (2002). The Antibiotic Paradox: How the Misuse of Antibiotics Endangers Their Curative Power. Da Capo Press, Cambridge, MA
# [http://whqlibdoc.who.int/HQ/2001/WHO_CDS_CSR_DRS_2001.10.pdf Mapendekezo ya Wataalamu wa Antibaotiki]
 
 
[[Jamii:Sayansi]]
Line 149 ⟶ 148:
[[sr:Антибиотик]]
[[sv:Antibiotikum]]
[[ta:நுண்ணுயிர் எதிர்ப்பி]]
[[ta:கிருமியெதிர்ப்பி]]
[[th:ยาปฏิชีวนะ]]
[[tl:Antibayotiko]]