Milano : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: bn:মিলান
No edit summary
Mstari 5:
 
== Historia ==
Mji ulianzishwa mnamo 400 KK na Wakelti ukawa mji wa Kiroma manmomnamo 222 KK ukajulikana kama Mediolanum. Mji ulikua katika [[Dola la Roma]]. Mwaka 293 [[Kaisari]] [[Diokletiano]] alichagua Milano kama mji mkuu wa nusu ya magharibi ya Dola la Roma. Tamko la MIlano lilitolewa 313 na makaisari Licinius na [[Konstantino Mkuu]] likatangaza mwisho wa mateso dhidi ya Wakristo.
 
Baada ya mwisho wa Dola la Roma katika magharibi mji uliharibiwa mara mbili na Wahunni na Waostrogothi wakati wa uhamisho wa Wagermanik. Ukatekwa tena na Walongobardi wahamiaji na kuwa mji mkuu wao. 774 uliingizwa katika himaya ya [[Karolo Mkuu]] ukaendelea kama sehemu ya falme za Wafranki, Wajerumani na [[Habsburg]] kwa karne nyingi.
Mstari 14:
 
== Umuhimu wa Milano katika Italia ==
Leo hii Milano ni mji wa pili katika Italia. Benki kubwa za nchi zina makao makuu hapa pia [[soko la hisa]] la Italia. Kuna viwanda vingi pamoja na kampuni ya magari ya [[Alfa Romeo]] na kampuni ya matairi [[Pirelli]]. Pia mji huu ni makao makuu ya vyombo vya habari mbalimbali kama Mediaset na magazeti kama Il corriere della sera. Mji huu pia ni kitovu cha michezo mbalimbali. Una uwanja wa Giuseppe Meazza (San Siro) wenye uwezo wa kubebe watazamaji zaidi ya 80,000 ambao ndio mkubwa kuliko vyote nchini Italia. Pia kuna timu mbili za mpira wa miguu, Inter na AC Milan ambazo ni moja ya vilabu vinavyoheshimika duniani. Milano huitwa mji mkuu wa mitindo ya mavazi ya Italia.
 
Mji unajulikana sana kwa [[opera]] yake inayoitwa "Scala". Jengo mashuhuri ni kanisa kuu au "duomo".