Atanasi wa Aleksandria : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Badiliko: es:Atanasio de Alejandría
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Sainta15.jpg|thumb|300px|right|[[Picha]] ya [[Atanasi wa Aleksandria]], [[Askofu mkuu]] ([[Patriarki]]) wa [[Aleksandria]] na mtetezi mkuu wa [[umungu]] wa [[Yesu Kristo]].]]
'''Atanasi wa Aleksandria''' anayeitwa ''Mkuu'' ([[295]] hivi - [[2 Mei]] [[373]]) alikuwa [[Askofu]] wa [[Kanisa Katoliki]] la [[madhehebu]] ya [[Misri]] aliyetetea [[imani]] ya [[Kanisa]] kati ya [[mitaguso ya kiekumene]] ya kwanza.
 
Anaheshimiwa kama [[mtakatifu]] na Wakatoliki, [[Waorthodoksi]] na [[Waorthodoksi wa Mashariki]]. Anakumbukwa pia katika kalenda ya [[Waanglikana]] na [[Walutheri]].
 
Wote wanaadhimisha [[sikukuu]] yake kila tarehe [[2 Mei]].
 
==Maisha==
 
Atanasi alizaliwa Aleksandria wa Misri mwishoni mwa [[karne III]], wakati [[dhuluma]] za [[Dola la Roma]] dhidi ya [[Ukristo|Wakristo]] zilizuwa zikielekea kilele halafu kikomo chake.
 
Alikulia katika [[jiji]] hilo, ambalo wakati huo lilikuwa likiongoza kimataifa upande wa [[ustaarabu]] na [[elimu]].
 
Upande wa dini, Wakristo wa Kimisri walikuwa na [[chuo]] muhimu, lakini kulikuwa pia na wafuasi wengi wa [[Gnosis]] na wa [[dini za jadi]] zilizoabudu [[miungu]] mingi.
Maisha yote ya Atanasi yanahusika na juhudi kubwa za [[Kanisa Katoliki]] kwa ajili ya kufafanua na kutetea [[imani sahihi]] juu ya [[Yesu]] na juu ya [[Utatu]].
 
Akiwa bado [[shemasi]] alimsindikiza [[askofu]] wake [[Aleksanda wa Aleksandria]] kwenye [[Mtaguso wa kwanza wa Nisea]] mwaka [[325]] ulioitishwa na [[kaisari]] [[Konstantino Mkuu]] kujadili mafundisho ya [[padri]] wa Aleksandria, jina lake [[Arios]], kuhusu dhati ya [[Yesu Kristo]].
 
Dhidi ya Arios, huo [[Mtaguso mkuu]] wa kwanza ulitumia neno la [[Kigiriki]] ὁμοούσιος (''homoousios'', yaani "wa dhati ileile"), ili kukiri kwa namna wazi usawa kamili wa [[Mungu Baba]] na [[Mwana]] aliyezaliwa naye bila ya kuumbwa.
 
Akishikilia msimamo huo moja kwa moja Atanasi alipaswa kustahimili dhuluma za serikali, hata akafukuzwa katika [[dayosisi|jimbo]] lake mara tano na kupelekwa uhamishoni tangu miaka michache baada ya kuchaguliwa [[Patriarki]] wa Aleksandria na wa Misri yote mwaka [[328]] (alipokuwa na umri wa miaka 30 tu) hadi mwaka [[362]].
 
== Maandishi ==
Line 30 ⟶ 46:
*[http://www.documentacatholicaomnia.eu/20_30_0295-0373-_Athanasius,_Sanctus.html Maandishi yake yote katika [[Patrologia Graeca]] ya Migne, pamoja na [[faharasa]] na [[tafsiri]] mbalimbali (EN, GR, LA, ES, RU)]
 
{{Walimu wa Kanisa}}
{{mbegu-Mkristo}}
 
{{Walimu wa Kanisa}}
 
[[Category:Waliozaliwa 295]]