Ambrosi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 6:
Anaheshimiwa kama [[mtakatifu]], [[babu wa Kanisa]] na [[mwalimu wa Kanisa]]. Sikuku yake ni tarehe [[7 Desemba]] kila mwaka.
 
==Maisha==
== Maandishi yake ==
===Mwanasiasa===
Ambrosi alizaliwa katika [[familia]] ya [[Ukristo|Kikristo]] ya [[Dola la Roma]] kati ya miaka 334 na 340 akakulia [[Trier]] ([[Ujerumani]]).
 
Baba yake, aliyeitwa Ambrosius Aurelianus, alikuwa [[liwali]] wa [[Gallia]] (leo [[Ufaransa]]); mama yake alijulikana kwa akili na imani yake. Ndugu zake, [[Satyrus]] na [[Marselina]] wanaheshimiwa pia kama watakatifu.
 
Alipofiwa baba, Ambrosi alifuata nyayo zake katika siasa. Alisomea [[Roma]], hasa [[fasihi]], [[sheria]] na [[hotuba]].
 
[[Liwali]] [[Anicius Probus]] kwanza alimpa nafasi katika halmashauri halafu akamfanya [[gavana]] wa [[Liguria]] na [[Emilia]], akiwa na makao makuu huko [[Milano]], mji wa pili wa [[Italia]].
 
Ambrose aliendelea na ugavana hadi mwaka [[374]] alipochaguliwa askofu wa Milano.
 
Ni kwamba, baada ya kifo cha [[Auxentius wa Milano]] aliyefuata [[uzushi]] wa [[Arios]], Ambrosi alikuwa amefika kanisani ili kutuliza ghasia kati ya [[Waarios]] na [[Wakatoliki]]. Lakini alipohutubia umati, akashangiliwa, "Ambrosi, askofu!". Alitaka kukataa, kwa kuwa hata hajabatizwa, lakini hatimaye alikubali.
 
Alipewa [[ubatizo]], [[kipaimara]] na [[ekaristi]], halafu baada ya wiki moja [[daraja takatifu]] ya [[uaskofu]].
 
===Askofu===
[[Image:Francisco de Zurbarán 032.jpg|thumb|left|120px|''Mt. Ambrose'', alivyochorwa na [[Francisco de Zurbarán]]]]
 
Kama askofu, zaidi ya [[useja]] wake, alishika juhudi za kitawa, alisaidia mafukara kwa mali zake karibu zote, akajitahidi kupata elimu ya [[Biblia]] na [[teolojia]] akaitumia vema katika kuhubiri.
 
Ilimbidi atetee [[imani sahihi]] dhidi ya wafuasi wa Arios, mmojawao [[kaisari]] aliyedai awaachie makanisa mawili ya Milano, lakini Ambrosi alikataa katakata, akisema,
"Ukinitaka mwenyewe, niko tayari kutii: unipeleke gerezani au kifoni, sitapinga; lakini sitasaliti kamwe [[Kanisa]] la [[Yesu Kristo]]. Sitaita watu kunisaidia; nitakufa kwenye [[altare]] lakini si kuikimbia. Sitahimiza watu kupiga kelele: lakini [[Mungu]] tu anaweza kuwatuliza.
 
[[Image:Anthonis van Dyck 005.jpg|thumb|300px|''Mt. Ambrosi na kaisari Theodosius'' walivyochorwa na [[Anthony van Dyck]].]]
[[Image:Sant'Ambrogio Cript in Basilica of Sant'Ambrogio, Milan.jpg|thumb|240px|right|Kikanisa chini ya [[basilika]] lake.]]
Ikulu halikupendezwa na msimamo wa Ambrosi, lakini ilimuogopa na kumhitaji katika mapambano ya siasa.
 
[[Theodosius I]], kaisari wa mashariki, alipoangamiza ([[390]]) watu 7,000 huko [[Thesalonike]] ([[Ugiriki]]), Ambrosi alitisha kumtenga na Kanisa asipofanya [[toba]] kama [[mfalme Daudi]], akamruhusu kupokea tena ekaristi baada tu ya miezi kadhaa ya malipizi.
 
Msimamo wake ulibaki kielelezo kwa Kanisa la magharibi hata likaendelea mara nyingi kushindana na serikali.
 
Ambrosi alipaswa pia kupambana dhidi ya [[Wapagani]] waliotaka kufanya tena [[dini]] ya jadi kuwa [[dini rasmi]] ya [[Dola la Roma]] badala ya Ukristo. Alifaulu kumfanya Theodosius I kutoa hati zake maarufu za mwaka [[391]].
 
Kati ya mambo ya pekee aliyoacha ni urithi wa tenzi na [[liturujia]] ya pekee inayoendelea kutumika Milano na sehemu nyingine za Italia kaskazini na [[Uswisi]] ("liturujia ya Kiambrosi").
 
Tarehe 4 Aprili Ambrosi alifariki, akaheshimika mara kama mtakatifu.
 
Masalia yake, ambayo ni kati ya maiti za zamani zaidi zilizopo nje ya [[Misri]], yanatunzwa katika kanisa lake mjini Milano.
 
== Maandishi yake ==
 
=== Ufafanuzi wa [[Biblia]] ===
Line 52 ⟶ 92:
* De obitu Theodosii
* Epistulae, hymni, etc.
 
==Vyanzo==
*Attwater, Donald and Catherine Rachel John. ''The Penguin Dictionary of Saints''. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-140-51312-4.
*[http://saints.sqpn.com/saint-ambrose-of-milan/ Patron Saints Index: Ambrose]
 
== Viungo vya nje ==
Line 57 ⟶ 101:
* [http://www.tertullian.org/fathers/ambrose_letters_00_intro.htm Barua za Mt. Ambrosi kwa [[Kiingereza]]]
* [http://www.documentacatholicaomnia.eu/20_40_0339-0397-_Ambrosius_Mediolanensis,_Sanctus.html Maandishi yake yote kutoka Patrologia Latina ya Migne pamoja na faharasa]
*[http://www.catholiclibrary.com/content/view/8575/5822/ Official Catholic Encyclopedia Live Article on St. Ambrose]
*[http://www.earlychristianwritings.com/fathers/ambrose_letters_00_intro.htm Early Christian writings: Letters of St. Ambrose of Milan]
*[http://www.ccel.org/fathers2/NPNF2-10/TOC.htm Christian Classics Ethereal Library, Works of Ambrose of Milan]
*[http://www.fh-augsburg.de/~harsch/amb_hy00.html Hymni Ambrosii (latin)]
*[http://www.earlychurch.org.uk/ambrose.php EarlyChurch.org.uk] Extensive bibliography
*[http://www.intratext.com/Catalogo/Autori/AUT12.HTM Ambrose's works]: text, concordances and frequency list
*[http://oll.libertyfund.org/Home3/AuthorBioPage.php?recordID=0011 Ambrose] at ''The Online Library of Liberty''
*[http://www.documentacatholicaomnia.eu/20_40_0339-0397-_Ambrosius_Mediolanensis,_Sanctus.html Opera Omnia]
*[http://www.mun.ca/Ansaxdat/ambrose ''Ambrose in Anglo-Saxon England, with Pseudo-Ambrose and Ambrosiaster''], Contributions to Sources of Anglo-Saxon Literary Culture, by Dabney Anderson Bankert, Jessica Wegmann, and Charles D. Wright.
*[http://www.aug.edu/augusta/iconography/ambrose.html "St. Ambrose" in ''Christian Iconography'']
*[http://www.cattoliciromani.com/forum/forumdisplay.php/liturgia_ambrosiana-59.html Forum about the "ambrosian rite"]
 
{{Walimu wa Kanisa}}
 
{{mbegu-Mkristo}}
 
[[Jamii:Waliofariki 397]]