Mtaguso Mkuu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Badiliko: la:Oecumenicum concilium; cosmetic changes
No edit summary
Mstari 4:
==Mitaguso saba na umuhimu wake==
 
'''Mitaguso ya kiekumene''' (''kutoka [[Kigiriki]] oικουμένη ''oikumene'' yaani ''dunia inayokaliwa na watu'') ni jina linalotumika hasa kwa mikutano saba ya namna hiyo iliyofanyika kati ya mwaka [[325]] hadi [[787]] upande wa mashariki wa [[Dola la Roma]] (ulioendelea baadaye kama Milki ya [[Bizanti]]).
 
Orodha yake ni kama ifuatavyo:
Mstari 26:
==Mapokezi ya mitaguso saba==
 
[[Mitaguso]] hiyo saba inakubaliwa hasa na [[Kanisa Katoliki]] na [[Waorthodoksi]], kutokana na msisitizo wao wa [[mapokeo]] na wa [[mamlaka ya kufundisha]] ya waandamizi wa [[mitumeMitume wa Yesu|Mitume]].
 
[[Makanisa ya kale ya mashariki]] hukubali mitaguso mitatu ya kwanza tu, na [[Kanisa la Waashuru]] ile miwili ya kwanza. Kukataa maamuzi ya mitaguso iliyofuata ndiyo sababu ya mafarakano yao.
 
Madhehebu kadhaa ya Kiprotestanti (hasa [[Walutheri]], [[Waanglikana]], [[Wamethodisti]], [[Wamoraviani]]) yanakubali mitaguso hiyo kadiri inavyolingana na uelewanouelewa wao wa [[Biblia]].
 
Hivyo Waprotestanti wengi wanashikilia imani juu ya [[Yesu Kristo]], juu ya [[Roho Mtakatifu]] na juu ya [[Utatu]] mtakatifu kama ilivyofundishwa rasmi katika mitaguso ya kwanza.
Mstari 78:
==Msingi wa imani kuhusu mtaguso mkuu==
 
Kadiri ya imani ya [[Kanisa Katoliki]], [[Yesu]] aliwakabidhi [[Mitume wa Yesu|Mitume]] kumi na wawili uongozi wa [[Kanisa]] wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani [[Mtume Petro]].
 
Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na [[Papa]] wa [[Roma]] ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye [[mamlaka]] ya juu katika Kanisa lote.