Katerina wa Bologna : Tofauti kati ya masahihisho

Mtawa wa Kiitaliano (1413-1463)
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Katerina wa Bologna''' ni jina linalotumika kwa kawaida kumtajia Katerina wa Vigri (8 Septemba 1413 - 9 Machi 1463), bikira na abesi wa ...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 07:52, 9 Mei 2010

Katerina wa Bologna ni jina linalotumika kwa kawaida kumtajia Katerina wa Vigri (8 Septemba 1413 - 9 Machi 1463), bikira na abesi wa Shirika la Mtakatifu Klara ambaye alitangazwa na Kanisa Katoliki kuwa mwenye heri tarehe 13 Novemba 1703 na mtakatifu tarehe 22 Mei 1712.

Mwili wake ulizikwa siku ya kufa kwake, lakini baada ya wiki mbili ulitolewa kaburini ukiwa haujaoza bali unanukia; baada ya matatizo mbalimbali uliwekwa kwenye kiti ambapo umeketi hata leo karibu na kanisa lake huko Bologna (Italia).

Bikira Maria na mtoto Yesu walivyochorwa na Katerina wa Bologna.

Maandishi yake

  • Le sette armi spirituali, Ed. Monastero del Corpus Domini, Bologna 1998;
  • I dodici giardini, Ed. Inchiostri Associati 1999;
  • Rosarium, Poema del XV Secolo, Ed. Barghigiani, Bologna, 1997;
  • I sermoni, Ed. Barghigiani, Bologna 1999;
  • Le Sette Armi Spirituali, Ed. del Galluzzo 2000;
  • Laudi, Trattati e Lettere, Ed. del Galluzzo 2000;
  • Corona de la Madre de Christo, Ed. Digigraf 2006.

Michoro yake

Kwa vipaji vyake vingi, Katerina alikuwa pia mchoraji mzuri. Kazi zake zinatunzwa sehemu mbalimbali za Italia.

Viungo vya nje