Prussia Mashariki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Prussia Mashariki''' ilikuwa jimbo la kihistoria katika dola la Prussia katika Ujerumani hadi mwaka 1945. Leo hii eneo lake limegawiwa kati ya mkoa wa K...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:02, 17 Mei 2010

Prussia Mashariki ilikuwa jimbo la kihistoria katika dola la Prussia katika Ujerumani hadi mwaka 1945. Leo hii eneo lake limegawiwa kati ya mkoa wa Kaliningrad wa Urusi na mkoa wa Warmia i Mazury katika Poland.

Prussia Mashariki ilikuwa chanzo cha Prussia yenyewe; tangu kuunganishwa na utemi wa Brandenburg ilikuwa tu jimbo la Mashariki. Mji mkuu ukawa Königsberg iliyoitwa leo hii kwa jina la Kirusi Kaliningrad.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na kuanishwa upya kwa dola la Poland Prussia Mashariki ilikuwa eneo la Kijerumani lisilo na njia ya moja kwa moja na nchi mama lakini mawasiliano wote yalikuwa kwa njia ya reli kupitia Poland au kwa njia ya bahari Baltiki.

Washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia walimaua kutenganisha jimbo hili na Ujerumani na kuigawa kati ya Poland na Urusi. Wenyeji wazalendo karibu wote walikimbia au walifukuzwa baada ya vita, kwa jumla watu milioni 2.5; wengi walikufa walipokimbia katika majira baridi ya Januari na Februari 1945.

Mwaka 1990 Ujerumani uliounganishwa tena ulikubali mipaka iliyotokea baada ya vita katika mapatano ya kimaaifa.