Chakula : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
nyongeza afya
Mstari 2:
[[Picha:FoodMeat.jpg|thumb|200px|Aina za [[nyama]].]]
 
Chakula ni kile kinacholiwa na watu kwa kudumisha maisha yao. [[Mwili]] unahitaji lishe, nishati na maji. Haya yote hupatikana katika chakula.
 
Mahitaji ya mwili ni hasa yafuatayo:
Mstari 17:
 
Kila nchi ina chakula chake na watu wamezoea vyakula pamoja na namna ya kutayarisha vyakula vyao.
 
==Chakula na afya==
Chakula kinatakiwa kuwa na sehemu zote zinazohitajika na mwili. Uhaba wa sehemu mmoja utasababisha magonjwa mbalimbali. Kuna matatizo hasa kama watoto hukosa chakula chenye ulinganifu. Mara nyingi wakinamama wanaowapa watoto chakula wanajali tu ya kwamba mtoto ashibe. Mtu anaweza kushiba kutokana na wanga pekee yake lakini uhaba wa protini na vitamini husababisha magonjwa na ikitokea kwa watoto upungufu wa kukua kwa sehemu za ubongo na mwili.
 
Vilevilekuna tatizo la mara kwa mara ni uhaba wa minerali fulani katika mazingira ya pekee.
 
Chakula kinahusiana na afya pia kuhusu uwingi au uhaba wake. Inaeleweka ya kwamba uhaba wa chakula yaani njaa kwa muda mrefu unadhoofisha mwili na afya. Lakini kinyume chake kuzidi kwa chakula kinaleta hatari pia. Katika maisha ya mjini na familia waliotoka katika umaskini kali hali ya [[kunona]] tangu utotoni imekuwa tatizo kubwa. Kunona kunafupisha maisha na kuandaa mwili kwa magonjwa mengi yasiyotokea kwa uzito wa wastani mwilini.