Gobori : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|300px|Muundo wa kimsingi wa gobori: 1: risasi 2: baruti 3: shimo la kupashia moto '''Gobori''' ni silaha ya moto asilia. Ni aina...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 20:32, 12 Juni 2010

Gobori ni silaha ya moto asilia. Ni aina ya bunduki ya kimsingi ambako risasi pamoja na baruti zinaingizwa pamoja kwenye mdomo wa kasiba ya silaha na risasi inafyatuliwa kwa kupasha moto kwenye shimo upande wa nyuma ya kasiba. Moto inawasha baruti na kusababisha mlipuko unaorusha risasi nje ya mdomo wa kasiba. Bunduki za kisasa hutumia ramia zinazopelekwa katika kasiba kutoka kando au nyuma.

Muundo wa kimsingi wa gobori: 1: risasi 2: baruti 3: shimo la kupashia moto

Hadi leo kuna aina kadhaa za mzinga zinazojazwa ramia kama gobori. Menginevyo gobori siku kizi ni silaha inayotengenezwa na watu nyumbani kwa uvindaji haramu au kwa michezo.

Kijeshi silaha hizi hazitumiwi tena tangu karne ya 20 kwa sababu matumizi yake ni ya polepole kulingana na bunduki za kisasa. Gobori inaweza kupigwa mara 1-2 kwa dakika si haraka zaidi kama askari ameandaa tayari mizigo midogo ya baruti tayari kwa kila safari ya kupiga. Bunduki zinazotumia ramia zinaweza kupiga mara nyingi kwa dakika.

Tazama pia

Viungo vya Nje