Ukanoni : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Ukanoni''' ni mtindo wa maisha ya kitawa uliokusudiwa hasa kwa mapadri wa parokia za mjini. ==Historia== Ili kuboresha maisha ya mapadri wanajimbo...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 04:31, 20 Juni 2010

Ukanoni ni mtindo wa maisha ya kitawa uliokusudiwa hasa kwa mapadri wa parokia za mjini.

Historia

Ili kuboresha maisha ya mapadri wanajimbo, toka zamani ulisisitizwa uundaji wa jumuia kati yao, ambamo wasali na kufanya utume kwa pamoja.

Hasa kuanzia karne XI wengi walifanya hivyo kwenye makanisa makubwa kama mtindo mpya wa kitawa unaosisitiza liturujia ya fahari pamoja na uchungaji.

Inavyoweza kueleweka, hao walifuata kanuni ya Agostino wa Hippo na kuitwa Wakanoni. Maarufu zaidi katika yao ni Norbert (1082-1134), mwanzilishi wa Wapremontree.

Leo mtindo huo unaendelea katika mashirika mbalimbali, ambayo lakini hayano watu wengi kama aina nyingine za utawa.